GE2025 Wagombea 14 wa Ubunge Jimbo la Mpina utata mtupu, Meatu wazua utata kwa wana CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Joined
Jan 30, 2023
Posts
74
Reaction score
80
Taarifa za CCM Mkoa wa Simiyu kuwa kuna wagombea 14 wa Ubunge Jimbo la Kisesa waliochukua fomu na Wagombea 13 jimbo la Meatu zimeibua sintofahamu kubwa na baadhi ya wanachama kudai kuwa wagombea ni wa mchongo ili kuvuruga mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama.

Minong'ono imekuwa mikubwa baada ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu kutaja orodha badala ya majina ya waliochukua fomu katika majimbo hayo.

Kwa upande wa Jimbo la Meatu watia nia wanajulikana ambao ni Salumu Hamis Salum (JAMBO), Leah Komanya, John Joseph, Donald Masunga, Luhende na Oscar Maduhu. sasa wananchi wanahoji hao wagombea 13 waliotajwa na Katibu Mwenezi wa CCM ni kina nani?

Kwa upande wa Jimbo la Kisesa, watia nia wanajulikana ni Michael Gambamala Luchunga, Mussa Mbuga, Lusingi Sitta, Wakili Silinde na Luhaga Mpina. hao wagombea wengine 14 wametoka wapi.

Kitendo cha Katibu Mwenezi wa Mkoa kuficha majina ya waliochukua fomu ni dalili za kutaka kuchomeka wagombea nje ya utaratibu na kuleta mpasuko mkubwa ndani ya Chama.

Ikumbukwe kabla ya Mpina hajachukua fomu ziliripotiwa taarifa kuwa hakuna mtu hata mmoja ambaye amechukua fomu Jimbo la Kisesa taarifa ambazo hazikuweza kukanushwa hadi Mpina alipochukua fomu ndio zikatolewa taarifa kuwa kuna wagombea 14.

View: https://www.instagram.com/p/DLhyL7dtfyJ/?utm_source=ig_web_copy_link

View: https://youtu.be/3xv7og0HWNw?si=XNj0XmxNfA5YQ3B0
 
Acha kelele wewe mleta mada majina sio lazima

Mbona katibu mwenezi taifa Makala kasema nchi nzima kuna wagombea ubunge 4.109 hakuwataja majina

Kataja idadi tu

Jiandae tu huko mbele utawajua vikao vikianza

Kuchukua fomu na kurudisha CCM ilitangaza hakuna upambe
Wamechukua fomu kimya kimya bila kelele wala kamera
 
Aliyeripoti nani? CCM? au uliokoteza taarifa mitandaoni? CCM inatoa tangazo baada ya wachukua fomu kukamilika .

Ulisikia CCM wakitoa tamko official? Kuwa hamna mtu?
 
Ccm wanataka kumpeleka mpina kugombea ACT-wazalendo urais kwa nguvu
 
Acha kelele wewe mleta mada majina sio lazima

Mbona katibu mwenezi taifa Makala kasema nchi nzima kuna wagombea ubunge 4.109 hakuwataja majina

Kataja idadi tu

Jiandae tu huko mbele utawajua vikao vikianza

Kuchukua fomu na kurudisha CCM ilitangaza hakuna upambe
Wamechukua fomu kimya kimya bila kelele wala kamera
Huwa tunawaambia CCM ni dude kuuuuuubwa sana!
 
Unakazana kumtoa mpina ili iweje?...
Amekufanya nini kibaya kiasi cha wewe kufikia hatua hii?.....
Roho ya kinyama sana...
Anyway muda utaamua!
 
Mkutano CCM wote walivaa nguo za CCM kasoro Mpina siku ile Samia anatangazwa mgombea

Jina Samia lilipotangazwa wajumbe wote walisimama kushangilia kasoro Mpina hakushangalia wala kuinuka kwenye kiti wala kupiga makofi

Ushahidi upo youtube

Tena aliinama chini kabisa kuwa he doesn't mind

Fikiria wajumbe wote wa mkutano mkuu wamevaa sare za CCM kasoro yeye tu

Inamaanisha nini? Anayejitenga na wenzie ni mchawi.Mpina mchawi sababu mkutano mkuu ule peke yake ndie alionyesha tofauti

CCM haihitaji wachawi na haipendi uchawi

Mpina hakuna kupita kakumbuka shuka asubuhi kujitia anavaa nguo za CCM baada ya kuona filimbi imepulizwa .

Kasahau ule mkuu hakuvaa nguo za CCM na hakuungana na wajumbe wengine nchi nzima kushangilia

Abaki hivyo kivyake ila sio CCM

CCM tunaheshimu maamuzi ya pamoja ya walio wengi

Aende zake huko
 
Taarifa za CCM Mkoa wa Simiyu kuwa kuna wagombea 14 wa Ubunge Jimbo la Kisesa waliochukua fomu na Wagombea 13 jimbo la Meatu zimeibua sintofahamu kubwa na baadhi ya wanachama kudai kuwa wagombea ni wa mchongo ili kuvuruga mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama.

Minong'ono imekuwa mikubwa baada ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu kutaja orodha badala ya majina ya waliochukua fomu katika majimbo hayo.

Kwa upande wa Jimbo la Meatu watia nia wanajulikana ambao ni Salumu Hamis Salum (JAMBO), Leah Komanya, John Joseph, Donald Masunga, Luhende na Oscar Maduhu. sasa wananchi wanahoji hao wagombea 13 waliotajwa na Katibu Mwenezi wa CCM ni kina nani?

Kwa upande wa Jimbo la Kisesa, watia nia wanajulikana ni Michael Gambamala Luchunga, Mussa Mbuga, Lusingi Sitta, Wakili Silinde na Luhaga Mpina. hao wagombea wengine 14 wametoka wapi.

Kitendo cha Katibu Mwenezi wa Mkoa kuficha majina ya waliochukua fomu ni dalili za kutaka kuchomeka wagombea nje ya utaratibu na kuleta mpasuko mkubwa ndani ya Chama.

Ikumbukwe kabla ya Mpina hajachukua fomu ziliripotiwa taarifa kuwa hakuna mtu hata mmoja ambaye amechukua fomu Jimbo la Kisesa taarifa ambazo hazikuweza kukanushwa hadi Mpina alipochukua fomu ndio zikatolewa taarifa kuwa kuna wagombea 14.

View: https://www.instagram.com/p/DLhyL7dtfyJ/?utm_source=ig_web_copy_link

View: https://youtu.be/3xv7og0HWNw?si=XNj0XmxNfA5YQ3B0

Kama Waziri Mkuu kaenguliwa,Mpina ni nani asienguliwe.
 
Back
Top Bottom