Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Wagombea 460 wajitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge Kagera zoezi la uchukuaji fomu lafungwa.
=========
Mchakato wa kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ulianza tarehe 14/07/2020 na kumalizika 17/07/2020 saa kumi jioni.
Katika mkoa wa Kagera wagombea 460 wa ubunge walichukua fomu na kuzirudisha na hivyo umebaki mchakato wa vikao vya mapendekezo.
Katika hao wagombea 460 ambao wamegawanyika katika sehemu mbili (wagombea wa viti maalum na wagombea wa majimbo) katika majimbo yote wagombea waliochukua fomu na kuzirudisha ni 404.
Na jumuiya wanayo jumuiya ya wazazi, vijana na UWT na wote wamefanya mchakato huu na kupata wagombea 56 na hivyo kufanya jumla ya wagombea 460 na mchakato ulifungwa rasmi tarehe 17/07/2020 na kubaki utaratibu wa vikao vya ndani vya mapendekezo.
Kuna majimbo 9 ya uchaguzi, Bukoba mjini wagombea waliochukua fomu na kuzirudisha ni 57, Bukoba vijijini wagombea 42, Muleba kaskazini wagombea 17, Muleba kusini wagomnea 52, Biharamulo wagombea 51, Ngara wagombea 43, Kyelwa wagombea 52, Karagwe wagombea 36 na Misenyi ( Nkenge)wagombea 54. Zoezi lilikamilika vizuri na hivyo taratibu za ndani ya chama zinaendelea.