Uchaguzi 2020 Wagombea 460 wajitokeza kuutaka ubunge Kagera kupitia CCM, milango yafungwa

Uchaguzi 2020 Wagombea 460 wajitokeza kuutaka ubunge Kagera kupitia CCM, milango yafungwa

Wagombea 460 wajitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge Kagera zoezi la uchukuaji fomu lafungwa.

=========
Mchakato wa kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ulianza tarehe 14/07/2020 na kumalizika 17/07/2020 saa kumi jioni.

Katika mkoa wa Kagera wagombea 460 wa ubunge walichukua fomu na kuzirudisha na hivyo umebaki mchakato wa vikao vya mapendekezo.

Katika hao wagombea 460 ambao wamegawanyika katika sehemu mbili (wagombea wa viti maalum na wagombea wa majimbo) katika majimbo yote wagombea waliochukua fomu na kuzirudisha ni 404.

Na jumuiya wanayo jumuiya ya wazazi, vijana na UWT na wote wamefanya mchakato huu na kupata wagombea 56 na hivyo kufanya jumla ya wagombea 460 na mchakato ulifungwa rasmi tarehe 17/07/2020 na kubaki utaratibu wa vikao vya ndani vya mapendekezo.

Kuna majimbo 9 ya uchaguzi, Bukoba mjini wagombea waliochukua fomu na kuzirudisha ni 57, Bukoba vijijini wagombea 42, Muleba kaskazini wagombea 17, Muleba kusini wagomnea 52, Biharamulo wagombea 51, Ngara wagombea 43, Kyelwa wagombea 52, Karagwe wagombea 36 na Misenyi ( Nkenge)wagombea 54. Zoezi lilikamilika vizuri na hivyo taratibu za ndani ya chama zinaendelea.
View attachment 1510190
Magufuli amekuza demokrasia ndani ya chama cha mapinduzi.

Kila mwenye shati la kijani na laki moja ya kuchezea ameweza kujipatia form ya kugombea ubunge.

Pongozi nyingi kwa chama cha mafisadi.
 
Huyo ni tycoon ndani ya ccm hakuna wa kumgusa labda ahamue yeye kutogombea na jambo ambalo haliwezekani
Ubunge kwake sio vijisent vya posho na mshahara ni fursa ya kuendesha biashara zake bila ya kubughuziwa na mtu
Ccm ipi? Hii ya jpm!?

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Wengi wanatafuta security ya mambo yao .Mabaya au Mazuri.Wattaalam wanasema ukiwa kiongozi CCM uguswi wala unyanyaswi na Mkuu wa wilaya wala Mkoa wala polisi.Sasa najiuliza sisi watu wakawaida nani anatulinda?JPM asipofanya mageuzi makubwa ya kiutawala ndani ya serikali yake private sector na serikali vitakuwa ni vitu viwili tofauti kwenye kujenga na kulinda uchumi.Anyway labda hii ndio style mpya wa utawala kwani kuna watu wanatengeneza vichaka vyao ndani ya CCM.
 
Ajira ngumu sana siku hizi hata wangefika 750 hakuna kushangaa
 
Huyo ni tycoon ndani ya ccm hakuna wa kumgusa labda ahamue yeye kutogombea na jambo ambalo haliwezekani
Ubunge kwake sio vijisent vya posho na mshahara ni fursa ya kuendesha biashara zake bila ya kubughuziwa na mtu
Naam.
Wewe ndo unamjua.

Hakuna wa kukata kura za maoni.
 
Nasikia Diwani wa Ijuganyondo kashinda CCM Manispaa katika watia nia
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa @innobash ametangazwa kuwa mshindi wa kura za maoni Jimbo la Karagwe, Kagera baada ya kupata kura 587 kati ya kura 679 zilizopigwa (86.5%), wagombea 34 walijitokeza kugombea katika jimbo hilo la karagwe. #MillardAyoUPDATES https://t.co/8xKduv4Eof
 
Back
Top Bottom