kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Wakuu amani iwe kwenu!
Bila kupoteza muda napenda kuzungumzia list ya wagombea 65 wanaodaiwa kutia nia kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Rorya. Hii list mara ya kwanza niliipata ikitokea kwa rafiki yangu aliyeko nchi ya China kwasasa ikiwa na majina 50 nilipopitia hayo majina nilipigwa na butwaa kubwa. Butwaa yangu ilinipelekea kutaka kujua ni nani hasa muandaaji wa hiyo list. Nilitaka kumjua muandaaji wa list ya wagombea hao na wala si kutaka kujiridhisha kama kweli watu hao wote wanagombea.
Unaweza kujiuliza kwanini nisingehangaika walau kujua kama hao watu wote wanagombea badala ya kutaka kujua muandaaji wa hiyo list. Nilitaka kujua hiyo list kwasababu moja kwa moja nilijua ile list si ya kweli, si ya kuaminika na mtu yeyote makini. Kwa haraka haraka niliwatambua wagombea 20 kwenye ile list tena kwa sura na makazi yao. Kwenye hiyo list kuna mkulima wa mboga mboga kando ya mto Mori (Nyanduga), kuna fundi baiskeli wa Mirare, kuna fundi ujenzi wa Malongo (Ingri Chini), kuna mfanyabiashara wa mbuzi (Ingri Juu), kuna mwanakwaya wa kigango cha Randa (RC), Kuna mvuvi mdogo wa samaki (Nyamagaro), kuna muuza duka wa Obwere (Shirati), kuna mwalimu wa Primary (Shule iko Kirumi). Hao ni baadhi ya watu nawajua vizuri na miji yao.
Ukiachana na hao watu niliyowataja wapo ambao hawajawahi hata kusika wakitaka kugombea ubunge mfano Mwalimu Ezekia Oluoch, Yupo La Kairo ambaye ndiye alikuwa mbunge huyu alitangaza kabisa siku wanazindua hospitali ya Wilaya kwamba hatagombea tena labda abadili gia angani pamoja na wengine wengi ambao kwanza hawajulikani na wala hawajawahi kutangaza nia. Pamoja na hao wapo pia wenye nia kweli ya kugombea akina Francsi Olweru, Wembe kwa uchachee.
Mara ya pili nilipotumiwa list hiyo nilishangaa sana kwamba sasa watu wameongezeka na kufikia 68 tena ikiwa hadi na jina la marehemu. Nipata majina ya rafiki zangu 5 tena wenye shughuli zao wala hawahaingiki na siasa, nilipowauliza kuhusu majina yao kuwepo kwenye watia nia wakabaki wanashangaa. Kilichonisikitisha ni kwamba muandaa list alisahau kuweka hata jina moja la mwanamke lakini kwenye list ya pili kuna dada moja.
Ile list imetoka wapi? ukweli ni kwamba simjui muanzilishi wa ile list ila kinachofanyika ni kwamba kuna jamaa moja aliipata ile list ikiwa na watu wachache tu kisha akaiedit kwenye whatsApp akamtumia mtu, huyo aliyetumiwa naye akaongeza watu wake akamtumia mtu na huyo mtu naye akaongeza basi ndiyo imekuwa hivyo hadi wakafika 68 na bila shaka watafika 100 maana naona hawajachoka kufanya hivyo.
Maoni yangu yako pale pale CDM wangemuweka Wenje Rorya au mgombea yeyote anayotokea Tarafa ya Nyancha mwenye ushawishi wangeshinda asubuhi sana. Ila hata Owawa bado anaweza akawapa CCM changamoto na wakisimamia kura zao vizuri wanaweza wakashinda pia.
All in all Rorya inahitaji mtu makini atakayeweza kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya Rorya mbele. Linapokuja suala la maendeleo ya Rorya basi RORYA KWANZA VYAMA BAADAYE SANA .Ndugu wapiga kura wa Rorya acheni kudanganywa na vikanga, kofia na virushwa vidogo vidogo mnavyopewa lakini zaidi acheni kumpa mtu kura eti kwasababu kawaletea mwanamuzi wa Ohangla kutoka Kenya.
la Kairo
Wewe ni rafiki yangu sana tena nimebahatika kufanya kazi kwako na hata kwenye kampeni zako nilishiriki sana ila ndugu yangu acha kulaghai wana Rorya kwa kuleta akina Osogo Winyo, Jackie Akinyi, na wanamuziki wengine kuwarubuni watu wa Rorya, unasababisha watu wapate UKIMWI bure, pili hizo hela mnazopanga kuhonga zikusanye mnunue hata ambulance isaidie wagonjwa.
Kindikwili- Masasi-Gongo la mboto-Shirati