GE2025 Wagombea ACT Wazalendo watoa tuhuma Uchaguzi Kura ya Mapema, ZEC yatoa ufafanuzi

GE2025 Wagombea ACT Wazalendo watoa tuhuma Uchaguzi Kura ya Mapema, ZEC yatoa ufafanuzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Baadhi ya wagombewa wa nafasi mbalimbali kupitia chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar wametoa tuhuma wakati wa utekelezaji wa zoezi la kura ya mapema ambalo limefanyika leo visiwani Zanzibar

Viongozi hao ambao ni pamoja na Omar Said Shaaban Mgombea Uwakilishi Jimbo la Pangawe pamoja na Mgombea Uwakilishi Jimbo la Malindi Ali Saleh wamesema miongoni mwa madai yao ni pamoja na kudai uwepo wa wapiga kura ambao hawahusiki na kura ya mapema kwa kudai kuwa wameveshwa sare za Vyombo vya ulinzi pamoja na sare za tume ya Uchaguzi ili kutekeleza zoezi hilo

Pamoja na hayo wagombea hao wamedai kuwa baadhi ya wapiga kura kutowekwa wino baada ya kukamilisha zoezi hilo jambo ambalo wamedai kuwa linaleta sitofahamu na kuondosha imani kwao

Akitoa ufafanuzi wa madai hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jaji George Joseph Kazi amesema kuwa Tume hiyo imehakikisha inazitatua dosari zilizojitokeza katika maeneo ya kupigia kura ili kutekeleza zoezi hilo kwa ufanisi

Kuhusu tuhuma za watu wengine kuveshwa sare, amesema madai hayo hayana uthibitisho kwani tayari katika kila kituo kuna orodha kamili ya wapiga kura ya mapema na katika vituo hivyo wako mawakala wa vyama vya siasa ambao wanafatilia mwenendo wa uchaguzi huo na kwa mujibu wa orodha iliyopo.

 
Walitegemea nini, wanapoteza muda tuu na pesa za walipa kodi, hakuna uchaguzi ni uhuni mtupu, binafsi sitapiga kura
 
ACT wameanza kusema "...yarabi tumeibiwa" tarehe 30 tutasikia MWIZI!!MWIZI HUYOOO!! kwi lwi
 
Unashirikiana na jambazi ukitegemea atakua mwema kwako baada ya kufanya ujambazi?
 
Back
Top Bottom