Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge wa CHADEMA walioenguliwa wapo zaidi ya wiki moja Dodoma Ofisi za Tume ya Uchaguzi

2 September 2020

Mwanasheria wa ACT Wazalendo atowa kauli kuenguliwa wagombea


2 Sep 2020
Mwanasheria Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Omar Said Shaaban, amefafanuwa mchakato wa rufaa za wagombea wa chama hicho walioenguliwa na wasimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Msikilize hapa.
Source : Weyani TV
 
CCM chama cha ujanja ujanja...yaani kama wanavyoishi madalali hapa mjini.
 
Kwanza kama ni kweli wamekosea ujazaji wa fomu,kwa nn kuwe na masharti magumu ya ujazaji kuliko kpind kingine chochote?
 
Kiukweli hapendezi kupita bila kupingwa bora waweke hata kivuli watu wachague Kati ya mgombea na kivuli
 
02 September 2020
Dodoma, Tanzania

Mgombea Monica Nsaro wa CHADEMA aelezea rufani yake aliyowasilisha Dodoma ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa zilizopo Dodoma


Monica T. Nsaro mgombea wa jimbo la Nzega Vijijini kupitia CHADEMA
 
2 September 2020
Dodoma, Tanzania

Mgombea wa CHADEMA awasilisha rufani Dodoma


Mgawe Ernest Stanley mgombea wa ubunge jimbo la Kibamba Ubungo Dar es Salaam yupo Dodoma ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa Taifa kufuatilia rufani yake.
 
Hivi kwa nini mnapenda kurejesha nyuma hili taifa? Hamna haya nyie? kujaza fomu tu ni mpaka atafutwe mwana sheria? Hivi kwa nini mnapenda kuwafanya wenzenu wajinga?
 
Hivi kwa nini mnapenda kurejesha nyuma hili taifa? Hamna haya nyie? kujaza fomu tu ni mpaka atafutwe mwana sheria? Hivi kwa nini mnapenda kuwafanya wenzenu wajinga?
Huu ni utaratibu wa ndani ya CCM na sio vyama vingine, vyama vingine wao wanajiamini kama watu wateule wao wanauwezo wa kujaza fomu. Matokeo yake wale walipitisha fomu kwa mwanasheria, fomu zao hazina kosa hata moja, na wale ambao hawakupitisha kwa mwanasheria, wao wana 50% ya makosa. Je ukiwa mwenyekiti wa chama chako itatafuta mchawi wapi, tume au uliowateuwa wako?

Mtu anaambiwa bandika picha mbele kwenye fomu hii, haweki. Jaza tarehe ya kuzaliwa, anaweka tarehe ya kupeleka fomu. Unategemea nini kitatokea?
 
Kujaza fomu ya udiwani na ubunge mnaweka wanasheria 1200!!!!???
Hao wabunge wanaojaziwa fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wataweza kuchangia miswada,kutunga sheria na kuisimamia serikali kweli!!???
 
Wewe ni kilaza,muongo na mbumbumbu. Weka ushahidi wa kiongozi wa upinzani aliyesema atamwaga damu.
Uongo ni ushetani na baba wa uongo ni shetani.
 
Dawa inachemka
 
Ulivyo mbumbumbu mwenyewe umeuliza "kwa nini ni upinzani tu ndio uonekane umekosea taratibu na kanuni za uchaguzi tokea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana. Maana yake umeuliza ni kwa nini iwe awamu hiii tuu!
Binadamu timamu lazima ajiulize,kwa nini ni awamu hii tu.
 

Post yangu namba #18 kwenye uzi huu inakupa majibu ya maswali yako.

Btw, ukatwaji umekuwepo tokea uchaguzi wa kwanza 1995, sio jambi geni. Rufaa za kabla ya uchaguzi na baada ya uchanguzi nazo zimekuwepo tokea 1995. Tatizo mitandao inaongozwa na vijana ambao aidha wavivu wa kumbukumbu, au hawakuwepo kwenye ulingo wa siasa za miaka ya zamani. Ndio maana wengi wanaona ni jambo la ajabu, lakini sio jambo la ajabu.
 
Yawezekana tume ina upofu na ukiziwi ina macho haioni ina maskio haisikii. Kuna nia ovu iliyokusudiwa si kwamba tume iko kimya pasipo sababu.
Mungu ibariki Tanzania, wape hekima wanaihusika ili amani, heshima na upendo visiangamizwe
 
Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa elimu kwa wagombea wao kwa wakati. Mtu anajaza jina lake kwenye sehemu ya tarehe ya kuzaliwa, unategemea msimamizi wa uchaguzi atafanya nini. Kama ni job interview, unategemea utaitwa tena?
Vyama vya upinzani hilo hawalioni kabisa.
Wakening semina chukka msimamizi wa uchaguzi awaseminishe maana ni haki yao.
Lakini huu ujuaji mtazidi kuumiza wananchi bure.
Na kulaumu wasimamizi.
 
Nimeona video ya mdada anaegombea Muheza na Mwana FA nikajua kwanini wapinzani hawataki wafanye kampeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…