Uchaguzi 2020 Wagombea uchaguzi huu hasa nafasi ya Rais njooni na suluhiso la ajira nchini, leteni sera za kuinua wawekezaji wa ndani

Uchaguzi 2020 Wagombea uchaguzi huu hasa nafasi ya Rais njooni na suluhiso la ajira nchini, leteni sera za kuinua wawekezaji wa ndani

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,192
Reaction score
5,685
Hello bosses,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Ni aibu kuona wanavyuo wengi wanahitimu wakati bado wengine wengi wako mitaani bila kazi au wanafanya kazi za chini sana ambazo hata hawakutegemea(kama vile ulinzi, vibarua, etc....)

Ni muda sasa wagombea wetu mje na sera za kutatua tatizo la ajira nchini.

Ni ukweli usopingika kuwa serikali kama serikali haiwezi kutatua hili swala peke yake, inahitaji msaada kutoka sekta binafsi nchini. Tatizo kubwa ni kwamba juhudi chache sana zimefanyika kuhamasisha uwekezaji wa ndani.

Sekta binafsi zikipewa sapoti kama vile misamaha ya kodi na sera zitakazorahisisha ufikiwaji wa raslimali zinazotakiwa na sekta hizo katika uzalishaji basi watu wengi tu wataajiriwa kwenye sekta binafsi hivyo kuondoa asilimia fln ya nguvukazi inayotumika sivyo mitaani.

Mfano mwingine ni kuhusu swala la Internet. Kiukweli internet ni kama ardhi ambapo kila mwenye nayo anaweza kuitumia kujiingizia kipato kwa namna anayoona iko sahihi(kimaadili na kisheria pia). Sasa nchini kwetu tunabanwa sana kiukweli katika matumizi ya mitandao. Ni wazi kuna watu wanaitumia vibaya, lkn kwa nini zisiwekwe namna nyingine tofauti na hizi kodi zilizowekwa na zinazoendelea kuwekwa kila mara. Kuna njia nyingi tu zinaweza patikana kuzuia matumizi mabaya ya mitandao ukiachana na kuwekewa kodi endapo wahusika wataamua kutafuta wataalam wakawapa ushauri.

Pia wanavyuo mnapokuwa mnalilia mikopo mkumbuke pia kuikumbusha serikali iandae mazingira mazuri ya kutatua swala la ajira lasivyo mtatukuta huku mitaani tunawasubiri muongeze namba ya tulio benchi.

Peace...
Kali Linux.
 
Back
Top Bottom