Uchaguzi 2020 Wagombea Urais msishangae kuonyeshwa makondokondo hadharani, Urais ni kama Sakramenti ya kufunga ndoa, lazima uwe msafi

Uchaguzi 2020 Wagombea Urais msishangae kuonyeshwa makondokondo hadharani, Urais ni kama Sakramenti ya kufunga ndoa, lazima uwe msafi

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Umuofia kwenu,

Huu ni mwezi wa kuchukua fomu, mtu yeyote kupitia chama anachokiamini anaweza kuchukua fomu ya kugombea urais, tofauti ni pale CCM walioamua kukinzana na katiba yao kuamua kumsimamisha mgombea wao huku wakizuia kujitokeza wengine wanaoweza kuleta upinzani, ambao baadhi yao walikimbia upinzani wakidai upinzani hakuna demokrasia.

Tune kwenye point. Ukiona moyo wako unakutuma kuwa unatosha kuwania urais, jua kuwa unawaandaa Watanzania watoe duduku yao kuwaonesha kuwa wewe ni msafi na umedhamiria.

Safari hii ni muda wa kutajana dhambi zote na kuzichambua kama zina maslahi mapana, kukusamehe ili upate ridhaa ya kuwatumikia wananchi. Lakini kama una makondokondo, hiyo fomu iondoe kabisa maana tunajiandaa kumwaga data za uwazi na ukweli.

Safari hii hatudanganyiki tena MTU mmoja kutuchagulia rais alafu akaja kutuumiza kama rule aliyetunga kitabu cha kutubu kwa aliyoyafanya akiwa rais. Au yule aliyesafishwa na chama cha upinzani kilichokuwa kinamnadi kama fisadi kuu alafu kikaja kuua iliyokuwa ajenda kuu ya ufisadi iliyokuwa inatumika kuisulubu CCM.

Vyama vyote vya upinzani kwa sasa havina ajenda kuu ya kuisimamia katika kukosoa utawala unaoondoka mwezi wa kumi.

Urais sio kifungo cha shati useme kikatika nitaweka kingine, urais usijaribiwe kwa kutaka umaarufu. Kwa sasa wanaejitokeza wachekeshaji weengi eti nao wanautaka. Nawaombeni sana rudisheni fomu za kujitoa kwani wiki ya kuchafuana imeanza. Zanzibar kushawaka moto wao huwa hawakopeshi wanakutwangia palepale.
 
Kuna mgombea mmoja ameshaweka bit maisha yake yasiongelewe. Cha kushangaza ni kuwa ni kwanini anajihami mapema?
Uzuri mitandao IPO wazi, wengi tutawawasha mtandaoni. Tunajua watajitetea kupitia vijigazeti walivyovianzisha.
 
Yule wa CCM si alisema kampeni za kumchokoza hataki.Yani na yeye ni mgombea halafu anawapiga biti anaoshindana nao.ani mwoga Kama kunguru huyu meko .Ila mwambie tunasubiri kukuche
 
Back
Top Bottom