Mmea Jr
JF-Expert Member
- May 20, 2016
- 798
- 1,871
Hodi hodi jukwaani ,, bila ya kupotezeana muda ,, moja kwa moja ningependa kudumbikia kwenye hoja ..
Najua fika ,, katiba ya nchii inamtaka mgombea wa kiti cha uraisi ,, awe na sifa zifuatazo ..
1) Awe raia halali wa nchi ya Tanzania...
2) Awe na akili timamu ..
3) Awe na umri usiopungua miaka 45 ..
4) Awe na chama kilichosajiriwa na kutambulika kisheria nchini.
Ok ,, sifa nilizozianisha hapoo juu ni sifa chache ,, miongoni mwa sifa nyingi zilizoanishwa na katiba ya jamuhuri ya muungano wa nchi hii ..
Sasa basi natambua fika yakuwa,, wagombea wengi wa kiti cha uraisi wa taifa hili ,, hupitia mchujo mzito ndani ya vyama vyao mbaka kuibuka kuchukua hatamu ya kuwa wawakilishi wa vyama vyao katika nafasi ya juu kabisa ya kugombea nafasi ya uraisi .. mchujo huu mzito huusisha mahojiano ,historia ya muuhusika kama vile utendaji wake kitaaluma toka akiwa mwanafunzi wa ngazi ya chini kabisa yani chekechea mbaka chuo kikuu ,, na hii uenda sambamba kabisa na kufuatilia historia ya tabia yake ilivyokuwa kipindi hicho akiwa mdogo mbaka kufikia hatua ya kuomba ridhaa ya kuwa raisi wa taifa hili kwani tumeshuhudia mara kadhaa walimu hata watu wao wa karibu waliowajua vyema wakihojiwa juu ya tabia ya wahusika pindi walipokuwa katika ngazi hizo za chini , pia utendaji wao wa kazi katika nafasi mbali mbali alizowahi zitumikia ndani au nje ya chama ,, ndani au nje ya serikali na mambo mengine mengi ..
Lakini wote nadhani mtakuwa mashahidi ,, baadhi ya hawa watu wanaopewa nafasi hii ya kuliongoza taifa wamekuwa wakionesha mapungufu fulani ,, inaweza kuwa katika namna wanaavyofanya maamuzi yao hasa juu ya maslai mazima ya taifa hili ,,, au katika namna wanavyopwaya katika nafasi walizomo ... Hivyo basi mimi ninawazo ,,
Kuwa hawa watu ,,, wanaogombea nafasi ya kuliongoza taifa hili ,, wasipimwe tu katika hoja zao wanazoziwasilisha kwetu sisi wananchi kipindi cha kampeni ,,, wasipimwe tu kwasifa za hapa na pale zinazotengenezwa na machawa wao ili tuwaone ni watu wanaofaa na wenye sifa za kuliongoza taifa hili ... Mimi napendekeza vigezo zaidi viongezwe na kimojawapo wawewanapewa mtiani wafanye ,,, ndiyo wafanye mtiani kwanini ??..
1) kwasababu ,, mfumo mzima wa taifa hili toka mwanzo umekuwa unapima ujuzi au uelewa wa mtu kwa njia ya mitiani ,,, toka la kwanza mbaka chuo kikuu,, tumekuwa tukiona na kusifia kuwa mtu mwenye akili na ulewa mpana ni yule anayepata alama za juu katika mitiani yake ,,, sasa kwanini tunapofikia katika ngazi hii ya kuliongoza taifa kipimo hichi kinafutwaa ??... Kama kipimo hichi hakitoa majibu sasa juu ya utandiji wa mtu kwanini tunakikumbania katika kazi hizi za chini ??
2) sasa hivi tumeona kuwa ili kupata kazi katika taifa hili ,,, imependekezwa kada zote zipitie kigezo cha kufanya mtiani kama moja ya sehemu ya mchujo .. hata zile ajira za mafungu kama ualimu na manesi mambo yamebadilisha ,, nao nasikia watatakiwa wafanye mtiani kama wenzao wa fani nyingine ... Sasa basi uraisi ni kazi kama zilivyo kazi nyingine ,,, sasa kwanini wanaoomba kazii hawapewi mtiani ili tuone ulewa wao kwa maslai mapana zaidi ya nchi ???
Wagombea ,, wapewe mtiani hata wa uraia tu wote waufanye na alama zao zitangazwe kwamba bwana mitomingi ngombalimwilu wa chama fulani kapata alama fulani,,, mimi nadhani hii itatupa picha fulani na itawasaidia sana wananchi kujua nani haswa anawafaa katika kuwaongoza kuliko kusikiliza polojo za mdomoni waziongeazo pindi wafanyapo kampeni .. najua na natambua watu watakao kuja kupinga hoja hii kwa kuniletea mifano ya mataifa yaliomdelea ambayo yameachana na mfumo huu wa mtiani kama moja ya kigezo kuhitimu au kufika hatua fulani... Lakini mimi nitawauliza watu hawa je,, katika hayo mataifa utaratibu wa mitiani umetolewa katika hatua moja tu au katika hatua zotee ?? Wana haiwezekani na haingii akili kama walimu ,, madaktari ,, mainginia ,, nk wote ndani ya taifa hili wanapatikana kwa kufanya mtiani ,,, afu katika nafasi hii ya juu mtu hapewi mtiani kwa visingizo mbali mbali ..
ASANTENI