Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,490
- 38,302
Heshima sana wanajamvi.
Tumeshuhudia vituko vya watia nia majimboni wakijaribu kucheza na akili za wananchi kwa kutumia siasa na hadaa za kijinga na utoto mwingi.
Innocent Bachungwa kaliacha V8 300 Land Cruiser nyumbani kachukua Corolla chakavu kwenda kuchukua form ya UBUNGE.
Pengine anataka kuwaadaa wananchi na wapiga kura yeye ni maskini mwenzao hana ukwasi wampatie tena nafasi ya ubunge kwasababu yupo kwaajili yao tu.
Kwa hakika anaweza kuwapata wajinga wajinga wakaamini kweli huyu ni mwenzetu lakini ni wazi hakuna Waziri katika awamu hii maskini.
Silinde huyu alikuwa CHADEMA akagundua huko hakuna hela kaamia CCM akatunukiwa Unaibu Waziri Mungu akupe nini !.
Silinde hapungukiwi vituko,jana kaenda kuchukua form ya ugombea UBUNGE kafika ofisi za chama na burungutu la hela Tsh 500,000 kwaajili ya kulipia form kaambiwa na Katibu eti BODA BODA walishamlipia yeye kazi yake ni kujaza tu hana haja ya kulipia hata ndururu !.
Tunawajua BODA BADO tunajua vipato vyao ni duni kweli kweli.Tunajua kazi yao ilivyo ngumu sokoni kupata abiria ni mparangano wa nguvu hawana tofauti na wapiga debe wanagombea abiria.
Eti wametoa 500,000 kwaajili ya mtu anayembelea V8 Land Cruiser 300 ?.Hao Boda boda wanataofauti gani na wale misukule ya Gerdavie wanao watoa sadaka wakati Nabii Mkuu anamiliki hadi Chopa waumini hata fedha za kupanda Daladala ni mshike mshike.
Kwa hakika Silinde na Bachungwa ni aina ya wanasiasa wajinga wanaotumia mbinu za kijinga kuwaadaa wapiga kura.Watanganyika tuwaepuke wanasiasa wa aina hii.
Ngongo kwasasa Kigoma Mjini.