Wagonga ulimbo mapenzi tuyaepuke kama ukoma

Wagonga ulimbo mapenzi tuyaepuke kama ukoma

kante mp2025

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
631
Reaction score
1,192
Nayasema haya nikiwa na simanzi moyoni hasa nikiwa katika wakati ambao mbili haisomi moja haisomi.

Hii naomba iwafikie wagonga ulimbo wote asee kama bado kula yako tu ni ya kuunga unga kama ngedere mapenzi yaepuke ikibidi uyakimbie kwa sauti ya nyanda kabudi mzee wa ogopaaaaaaa

Amesema hanitaki mbele ya majirani na wanazengo imeniuma sana ila imenipa bonge moja la motivation huyu mwanamke kasema nitafute sana pesa ndio kauli ya mwisho kuniambia huku akifyonya.

Mimi ni Mhehe kwa kabila ila siwezi kujinyonga kuna mama mwenye nyumba hapa kanambia mwanangu Mungu anavokuletea baraka kuna nuksi huwa anaziondoa kwa namna usiyoitegemea hivo usihuzunike kijana wangu huwezi jua Mungu kakupangia nini.

Maneno haya yamenitia moyo hapa nasikiliza kibao cha zamani cha mbarakah mwinshehe nilikuwa nakisikiza kwenye redio mbao kwetu kijijini kuna verse inasema

kasema hakutaki japo aliimbiwa mwanamke naona kama nasemwa mimi
 
Tafuta hela ili uweze kuondoa shida zako, usi tafute hela ili uka honge mwanamke.
FB_IMG_17390485416712649.jpg
 
Back
Top Bottom