maufoungph
Member
- Oct 16, 2018
- 77
- 171
Wagonjwa wa kifua kikuu (TB) hupitia mateso makubwa ambayo mara nyingi jamii haioni. Si kwamba wanapenda kuacha dawa au kuzembea matibabu yao bali mara nyingi huzuiliwa na hali halisi ya maisha. Daktari anapomwambia mgonjwa wa TB kwamba hatakiwi kufanya kazi kwa miezi sita au zaidi maana yake ni kwamba mgonjwa huyo anakuwa tegemezi kwa kila kitu chakula,mavazi,usafiri hata mahitaji madogo ya kila siku.
Hapa ndipo mateso makubwa huanzia. Familia nyingi hukimbia jukumu la kuwatunza. Marafiki hujitoa. Jamii inatazama kwa mbali kana kwamba wagonjwa hawa wameshawekwa nje ya mzunguko wa binadamu. Wengine hata hukimbizwa maneno ya dharau na unyanyapaa kana kwamba TB ni laana. Mgonjwa ambaye tayari anahangaika na maumivu ya mwili na mzigo wa dawa kali,anaongezewa mzigo mwingine wa mateso ya kisaikolojia na upweke.
Ni kweli kwamba dawa za TB zipo bure hospitalini lakini dawa peke yake haziwezi kumponya mgonjwa anayekosa mlo wa uhakika. Kila anayefahamu matibabu ya TB anajua kwamba dawa hizi ni nzito mwilini na haziwezi kumezwa tumboni pasipo chakula. Mgonjwa anapokosa msaada wa chakula maana yake ni kifo kinachosababishwa si na ukosefu wa dawa bali na ukosefu wa utu na mshikamano wa kijamii.
Kuna wagonjwa wengi wanaotelekezwa na kuachwa wafe kimya kimya kwenye vyumba vyao vya giza. Wanaishi kwa hofu,wakiwa na machozi na mwili unaokonda siku baada ya siku. Hakuna anayejali. Hakuna anayewajali. Hii ndiyo taswira halisi ya ukatili wa jamii yetu leo. Jamii ambayo haioni thamani ya maisha ya wanyonge.
Kifua kikuu si hukumu ya KIFO iwapo mgonjwa atapatiwa msaada sahihi. Lakini bila msaada wa chakula,heshima na huduma ya karibu matibabu hayaendi popote. Tunapaswa kujiuliza: inakuwaje familia nzima au jamii nzima ikashindwa kushirikiana kumsaidia mtu mmoja kwa kipindi cha miezi sita tu ili aokoke na kurejea kuwa mwenye nguvu tena?
Leo hii ukimya wetu unawaua wagonjwa wengi zaidi kuliko TB yenyewe😭. Jamii inaposhindwa kuwahudumia wagonjwa wake basi sisi sote tumeshiriki kwa njia moja au nyingine katika KIFO chao.
Msaada mdogo tu sahani ya chakula,maneno ya faraja,msaada wa usafiri kwenda kliniki unaweza kuwa daraja kati ya maisha na KIFO kwa mgonjwa wa TB. Wacha tuache kugeuka pembeni. Wacha tuache kuwatupa wagonjwa hawa. Wacha tuguswe na ubinadamu,kwani kesho inaweza kuwa sisi au ndugu zetu.