Wagonjwa wa "Red eyes" muwe wastarabu

Wagonjwa wa "Red eyes" muwe wastarabu

Upo sahihi kwa kila kitu ila huu ugonjwa husababishwa na virusi (at least hicho ndicho walichobandika ukutani)

Nafikiri ndiyo maana hata kupona kwake ni kwa kujichunga kwa kunawa maji mara kwa mara, kukaa eneo ambao halitakazia ugonjwa n.k. nahisi ingekua bacteria kupona ingekua rahisi. Kwakua hauui wafanyakazi wamejiambukiza makusudi na kuomba leave na wamegewa
 
Jana nilipita sehemu nikamuona mchoma maindi kavaa zake miwani mikubwa meusi (kimoyomoyo nikajiambia atakuwa na red eyes tu huyu). Mara akanyanyua kidogo miwani akaanza kufikicha macho, jicho jekunduuu.
Then akaendelea kuzungusha zungusha maindi bila hata kunawa.
Mungu atusaidie tu kwa kweli, na maisha yetu yalivyo magumu hata kama unaumwa lazima utoke uhangaike!!
 
Poleee Mkuu, ila nimechekaaa....🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Hao wanaoambukiza wenzao makusudi ni wale tuumwe wote tuteseke wote..... kiukweli si ustaarabu.

Ila hao uliowakuta wako kazini na miwani yao, sidhani kama wamependa. Ukute bosi kawaambia usipokuja kazini ukipona ukatafute kazi mahala pengine.

Naamini hakuna asiyependa kupumzika, labda wawe wanavizia tipu njaa. Ila wanaofanya vibarua ili walipe bili zao za kila siku hawanauthubutu wa kujiamlia kupumzika.

Umenikumbusha enzi nafanya kazi, si kuwa nilikuwa napenda kufanya kazi ila mafua/flu yalikuwa hayanilazi nyumbani.

Safari moja yalikomaa, niko kwenye dawati la kazi, uso umenivimba, mwili wa moto, mafua yanachuruzika kama maji, bosi wangu akaniambia... Kasinde nenda nyumbani ukipona ndo uje....

Sikuwa mtu wa vizinga vya ruhusa za kila leo... hivyo siku nikiomba udhuru ujue kweli nimekamatika.

Poleni asieeh, ila kujikinga na wewe vaa tuu hiyo miwani tintedi ili miale ya redeye isikupate.
Umeacha kazi? Unafanya shughuli gani now?
 
Jana nilipita sehemu nikamuona mchoma maindi kavaa zake miwani mikubwa meusi (kimoyomoyo nikajiambia atakuwa na red eyes tu huyu). Mara akanyanyua kidogo miwani akaanza kufikicha macho, jicho jekunduuu.
Then akaendelea kuzungusha zungusha maindi bila hata kunawa.
Mungu atusaidie tu kwa kweli, na maisha yetu yalivyo magumu hata kama unaumwa lazima utoke uhangaike!!
kukosa elimu ya kutosha pia inachangia
wengi sana wanajua unapata huo ugonjwa ni kwa kuwa zamu yako imefika

binafsi wakati nasoma chuo cha kati, dorm karibia lote liliumwa, mie sikuupata sababu tu nilikataa kupeleka mikono machoni
 
Hebu ona sasa. Mtu anajua kabisa anaugonjwa wa macho halafu anachoma mahindi. Imagine idadi ya watu wengine atakaowaambukiza na kuwalisha uchafu.

Ukiona sehemu ya mtoa huduma mtu kavaa miwani myeusi kama paka wa kichawi jua tayari anasumbuliwa na red eyes.
 
HUO NDIO UAFRIKA, LAANA NA KOSA KUBWA ALILOLIFANYA mUNGU (KAMA YUPO) NI KUMUUMBA MTU MWEUSI
Kwahiyo mjomba hao mashoga mnaowashabikia hawana laana sio! Nyinyi ndio wale nyimbo ya lil wayn anawazungumzia masnitch kwenye jamii yake lkn bado mkija humu mnasema waafrica ndio masnitch
 
kukosa elimu ya kutosha pia inachangia
wengi sana wanajua unapata huo ugonjwa ni kwa kuwa zamu yako imefika

binafsi wakati nasoma chuo cha kati, dorm karibia lote liliumwa, mie sikuupata sababu tu nilikataa kupeleka mikono machoni
Kabisa mkuu, ukikaa vijiweni utasikia wanajibizana "subiri zamu yako itafika". Kumbe inabidi uweke viganja vyako mbali na macho.
Sasahivi hata door handles hatushiki kwa viganja, tusukumizia chini tu na viwiko!
 
Hebu ona sasa. Mtu anajua kabisa anaugonjwa wa macho halafu anachoma mahindi. Imagine idadi ya watu wengine atakaowaambukiza na kuwalisha uchafu.

Ukiona sehemu ya mtoa huduma mtu kavaa miwani myeusi kama paka wa kichawi jua tayari anasumbuliwa na red eyes.
Ndio maana kuna watu hawali vyakula vya barabarani.
 
Kwahiyo mjomba hao mashoga mnaowashabikia hawana laana sio! Nyinyi ndio wale nyimbo ya lil wayn anawazungumzia masnitch kwenye jamii yake lkn bado mkija humu mnasema waafrica ndio masnitch
ushoga wao is none of your business! ni mambo ya chumbani kwao hayakuhusu, tunasema those issues that impact everybody's daily life
 
Habarini wadau.

Kuna maambukizi ya ule ugonjwa wa macho mekundu almaarufu kama red eyes, ambao husababisha macho kuwasha, kuuma, kuwa mekundu sana, kuvimba na kutoa uchafu mwingi sana wa tongo tongo.

Ni ugonjwa unaosambaa kwa kasi sana endapo tahadhari hazitachukuliwa mapema kutoka kwa walio ambukizwa kuwaelekea ambao hawajaambukizwa.

Ugonjwa huu unasambaswa sana kwa njia ya vimelea au Virusi kutoka kwa mgonjwa anaposhika macho yake na kuwapakaza wengine kwa njia ya kuwagusa aidha machoni direct (hii ni kwa watoto sana sana maeneo yao ya michezo), au mgonjwa kujigusa machoni wakati akijifikicha na kushika sehemu mbali mbali kama vitasa vya milango, siti za daladala na mabomba ya abiria waliosimama na kujishikiza, vijiko, sahani, vikombe au glass, remote , na hata arm rest za viti wanaposhika na kupakaza wale Viruses, kushikana mikono wakati wa salam na kadhalika.

Kitu kinacho nikwaza katika kipindi hiki cha maambukizi ni changamoto ya watu ambao tayari wameambukizwa inakuta wanajichanganya maeneo ya mkusanyiko na miwani yao myeusi kama paka wa kichawi wakishika vitu, pesa, na mazingira kwa ujumla jambo linalopelekea kusambaa kwa Virusi hawa wabaya kwa kasi kubwa.

Imagine pesa inashikwa na mikono michafu mingapi ya watu wenye red eyes wasio na ustaarabu wa kunawa mikono yao na sabuni ili kupunguza maambukizi.

Unakuta jitu linafikicha macho halafu linashika vyombo, milango, pesa, na kusababisha Virusi kusambaa kwa kasi.

Kwann usitulie nyumbani japo hata siku mbili au tatu ujiuguze upone ndipo kujichanganya na watu, au kama ni lazima sana kutoka why usichukue tahadhari ya kubeba sanitizer mfukoni au kwenye pochi, na kusanitize mikono yako kila baada ya masaa kadhaa ili kupunguzo carriage load ya Virusi kwenye viganja na vidole vyako before haujasambazia wengine popote walipo?

Kwann usiwe na subira na afya yako at least upone kwanza kabla haujawasambazia wengine?

Tahadhari ni muhimu ili kuwalinda wengine, mtu una mgahawa unaruhusu vipi muhudumu au mpishi aje kazini na anaumwa red eyes kwann usimpe 'paid leave' hadi apone ndipo aje kazini?

Mtu anahudumia watu huku kavaa miwani myeusi, macho yamevimba na machafu yanatia kinyaa hata kutazama. Why unaendelea kukaa eneo la kazi badala ya kujiuguza at least upate nafuu.

Aisee nimechefukwa sana leo. Nimekuna na watu wenye red eyes sehemu 4 tofauti na pote huko wanashika shika vitu na pesa. Nimechefukwa sana aisee.
Nini Hatua nifanye kama sijaambukizwa
 
Upo sahihi 60% na haupo sahihi 40%

Kinachomsumbua MTU mweusi siku zote ni ubinafsi ule wa akiwa anaumwa basi tuumwe sote na akiwa masikini basi tuwe masikini sote.

Red eyes inasambazwa makusudi MTU anaumwa Ila anataka Ku-shake hands na kila MTU .
 
Riziki ya mbwa ipo kwenye miguu yake. Kama wewe ni mbwa wa kufugwa huwezi jua hili.
 
Back
Top Bottom