Wagonjwa wa saratani 30,000 wanapoteza maisha kila mwaka

Wagonjwa wa saratani 30,000 wanapoteza maisha kila mwaka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Dr Kingwangila.jpg


Kwa ufupi
  • Imedaiwa kwamba wagonjwa wanaopoteza maisha ni wale waliofikiwa hatua za mwisho
By Pamela Chilongola,Mwananchi pchilongola@mwananchi.co.t


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kingwangalla amesema kila mwaka wanapokea wagonjwa wa saratani 40,000 kati ya hao 30,000 wanapoteza maisha.

Anasema wagonjwa wanaofikishwa katika Hospitali ya Ocean Road wanakuwa kwenye hatua ya mwisho ambapo saratani inakuwa imeshasambaa.

Dk Kingwangalla amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 7 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa wataalamu wa tiba ya mionzi ambapo nchi 17 za Afrika zinashiriki.

Kingwangalla amesema idadi hiyo ya wagonjwa inasababishwa na watu kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara.

“Watu wanaoenda kwenye vituo vya afya ni asilimia 25 tu na hii inachangia uelewa ni mdogo hivyo wanatakiwa waje hospitalini kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kujijua kama wana tatizo au la, ”alisema na kuongeza:

“Lakini kinachojitokeza wengi wao wanaenda kwenye vituo vya afya vya kawaida ambavyo haviwezi kugundua ugonjwa wa saratani,”alisema Dk Kingwangalla .
chanzo.Wagonjwa wa saratani 30,000 wanapoteza maisha kila mwaka

Hata kama Wagonjwa wa Saratani watakuja kupimwa Mheshimiwa Dk Hamisi Kingwangalla hakuna dawa Hospitalini za kuweza kuwatibu Wagonjwa wa Saratani watakufa tu. Dawa za asili zipo na zinaweza kuwatibu wagonjwa wa Saratani na wakapona.
 
Wakati nimgumu sana!!! labda tusubri carine nyingine tunauna tunaona na kujua. nayasema haya kwa masikitiko makubwa sana je? tulimkosea nini Mungu ??? Tanzania siri zinasemwa ukweli unafichwa!!
 
Back
Top Bottom