Wagonjwa watakiwa kufua mashuka ya hospitali

Wagonjwa watakiwa kufua mashuka ya hospitali

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ukosefu wa maji katika Kijiji cha Chihangu kilichopo Wilaya ya Newala, Mkoa wa Mtwara umesababisha wagonjwa wanaotibiwa katika Kituo cha Afya Chihangu kutakiwa kufua nguo za hospitali kabla ya kuruhusiwa.

Mkazi wa Kijiji cha Kihangu B, Musa Kajana amesema wagonjwa wanapomaliza kupata matibabu wamekuwa wakitakiwa na kituo hicho cha afya kufua shuka wanazozitumia ili waziache zikiwa safi.

“Huwezi kuruhusiwa hapa mpaka ufue shuka kwa kutumia maji yako ndio uyarudishe, shuka zinakuwa hazina madhari nzuri sababu ya uchafu, ndio maana wagonjwa wanakataa kutumia shuka za hapa,” amesema Kajana.

Wananchi hao wameeleza kero wakati wakipokea msaada wa mashuka 100 na vitanda kumi na magorodo kumi vyenye thamani ya Sh7 milioni vilivyotolewa na Benki ya NMB wilayani Newala.

Mkuu wa kituo hicho, Dkt Anthony Rioba amesema wakati wa changamoto ya maji waliwaomba wagonjwa hususan wale wa upasuaji kusuuza nguo za hospitali ambazo zinakuwa zimechafuka damu na uchafu mwingine kisha wao hospitali huzifua kwenye mashine na dawa.

Waziri wa nchi, ofisi ya Rais, (kazi maaluum), George Mkuchika ambaye amepokea msaada huo kutoka NMB amesema Serikali imetoa kiasi cha Sh84 bilioni kwa ajili ya kukarabati mradi wa makonde na tayari wakandarasi wapo kazini wilayani Newala.

“Kwa hiyo ndugu zanguni kwa shida ya maji ilivyotusumbua sasa neema inakuja, mradi wa Makonde ni wa muda mrefu toka mwaka 1953 mitambo imechoka, mabomba yameoza na uzalishaji umekuwa mdogo sana”.

Mkazi wa Chihangu, Celestine Nandonde, ameiomba Serikali kuharakisha mradi huo ili msaada wa mashuka uliotolewa na NMB uwe na manufaa na yaweze kuwa katika hali nzuri.

MWANANCHI
 
CCM mnatesa wananchi. Miaka 61 ya uhuru bado maji mmeshindwa kuwapatia wananchi wenu?

Siku hizi naona hadi IGP ana msafara wa Land Cruiser V8 tatu. Hizo si bora bora zisiwepo hela mlachimbie visima vifupi, vya kati na vitefu?
 
Bujibuji una Mawazo mazuri Sana, nani atakuelewa? Kama wanamaji wa ziwa viktoria mitungi haikuwa na oksijeni wakati wananunua v8 mil 500 unafikiri wanajielewa? Wala hawana utu hawa maccm! Ile ajali imekuwa ni aibu kwetu dunia nzima, tunanuka kila mahali. Ila mishipa ya aibu ilishakatika kwa hiyo hatujali kabisa!
 
Hizo posho wanazojilipa sasa!!!! Ni balaa.
Mama yuko busy sana kuzunguka dunia akiwa na msafara mkubwa sana kutafuta hela ambazo zinakuja kupigwa
 
Back
Top Bottom