John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Taarifa za mwaka 2021 kutoka kanzi data ya wagonjwa iliopo Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inaonesha kuwa Saratani zinazoathiri wanaume zaidi ni:
Saratani ya tezi dume“Prostate cancer” (21%), Saratani ya Koo (Esophageal Cancer) (11.8%),Saratani ya utumbo mkubwa na mdogo (9%) na Saratani ya mdomo na kinywa (7.3%) na kwa upande wa wanawake saratani zinazowaathiri zaidi ni pamoja na Saratani ya Mlango ya Kizazi (Cervical Cancer) (43%), Saratani ya Matiti (Breast Cancer) (14.2%) na Saratani ya koo (3.8%).
Siku ya Saratani Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 4 Februari. Siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka 2000 mjini Paris, Ufaransa wakati wa mkutano wa Dunia wa saratani na ni maalumu ili kutoa elimu ya kinga na kuelimisha wananchi na serikali hatua za kuchukua kukabiliana na ugonjwa huu. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani kwa mwaka 2022 ni: ‘(Huduma za saratani sawa kwa wote) '