Oltung'anyi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 284
- 196
Wahadhiri wengi wa vyuo vikuu siyo waalimu kitaaluma. Wengi hupata fursa ya kufundisha vyuo vikuu kwa kuwa walipata GPA ya first class au kupitia uzoefu wa kazi kulingana na taaluma yake.
Ifahamike kuwa, sio tu kufundisha kile mtu ajuacho au kukiamini, lakini pia hata namna ya kukifundisha(the art of teaching) ni muhimu sana.
Binafsi ninajikuta katika lundo la tafakari pale ninapoona mtu anakabidhiwa jukumu la kufundisha ati kwa kuwa amefaulu vizuri masomo bila kujali kuwa ualimu ni taaluma na siyo kila mmoja anaweza kuchukua jukumu hili lenye kuhitaji mchakato wa muda mrefu wa mafunzo kabla ya kupewa jukumu la kufundisha.
Labda ndio mfumo na vigezo vipo vya kuganya hivi, na pengine wahadhiri si waalimu na labda huwa wanapewa mfunzo ya ziada ya ualimu. Wenye ufahamu zaidi watujuze.
Naombeni tulitazame jambo hili kwa kina wadau. Binafsi ninaona madhara ya kufundishwa na Wazoefu wa kazi na wenye ufaulu wa juu. Kuna Ulipuaji mkubwa sana. Wahadhiri wanabaki kuhodhi maarifa tu na kuwanyanyasa wanachuo.