Wahadhiri na Mustakabali wa Elimu

Wahadhiri na Mustakabali wa Elimu

Oltung'anyi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
284
Reaction score
196
Wahadhiri wengi wa vyuo vikuu siyo waalimu kitaaluma. Wengi hupata fursa ya kufundisha vyuo vikuu kwa kuwa walipata GPA ya first class au kupitia uzoefu wa kazi kulingana na taaluma yake.

Ifahamike kuwa, sio tu kufundisha kile mtu ajuacho au kukiamini, lakini pia hata namna ya kukifundisha(the art of teaching) ni muhimu sana.

Binafsi ninajikuta katika lundo la tafakari pale ninapoona mtu anakabidhiwa jukumu la kufundisha ati kwa kuwa amefaulu vizuri masomo bila kujali kuwa ualimu ni taaluma na siyo kila mmoja anaweza kuchukua jukumu hili lenye kuhitaji mchakato wa muda mrefu wa mafunzo kabla ya kupewa jukumu la kufundisha.

Labda ndio mfumo na vigezo vipo vya kuganya hivi, na pengine wahadhiri si waalimu na labda huwa wanapewa mfunzo ya ziada ya ualimu. Wenye ufahamu zaidi watujuze.
Naombeni tulitazame jambo hili kwa kina wadau. Binafsi ninaona madhara ya kufundishwa na Wazoefu wa kazi na wenye ufaulu wa juu. Kuna Ulipuaji mkubwa sana. Wahadhiri wanabaki kuhodhi maarifa tu na kuwanyanyasa wanachuo.
 
Hii ndivyo ilivyo duniani, si Tanzania tu bali popote uendapo, shurti Mhadhiri awe amefaulu vyema, yani GPA iliyosimama khasaaa.

Asante
 
Hii ndivyo ilivyo duniani, si Tanzania tu bali popote uendapo, shurti Mhadhiri awe amefaulu vyema, yani GPA iliyosimama khasaaa.

Asante
Ninakusoma ndugu, suala kubwa hapa ni kuwa si kila mtu anaweza kuelekeza/kufundisha. Bila shaka ufundishaji ni taaluma na pengine si kila mtaaluma wa fani yoyote anaweza kuifundisha fani hiyo. Hili ndilo suala ninaloliangalia zaidi.
 
Wahadhiri wengi wa vyuo vikuu siyo waalimu kitaaluma. Wengi hupata fursa ya kufundisha vyuo vikuu kwa kuwa walipata GPA ya first class au kupitia uzoefu wa kazi kulingana na taaluma yake.

Ifahamike kuwa, sio tu kufundisha kile mtu ajuacho au kukiamini, lakini pia hata namna ya kukifundisha(the art of teaching) ni muhimu sana.

Binafsi ninajikuta katika lundo la tafakari pale ninapoona mtu anakabidhiwa jukumu la kufundisha ati kwa kuwa amefaulu vizuri masomo bila kujali kuwa ualimu ni taaluma na siyo kila mmoja anaweza kuchukua jukumu hili lenye kuhitaji mchakato wa muda mrefu wa mafunzo kabla ya kupewa jukumu la kufundisha.

Labda ndio mfumo na vigezo vipo vya kuganya hivi, na pengine wahadhiri si waalimu na labda huwa wanapewa mfunzo ya ziada ya ualimu. Wenye ufahamu zaidi watujuze.
Naombeni tulitazame jambo hili kwa kina wadau. Binafsi ninaona madhara ya kufundishwa na Wazoefu wa kazi na wenye ufaulu wa juu. Kuna Ulipuaji mkubwa sana. Wahadhiri wanabaki kuhodhi maarifa tu na kuwanyanyasa wanachuo.

Acha kujichanganya. Unaongelea taaluma mbili tofauti uhadhiri na ualimu. Kazi ya wahadhiri ni kutoa mihadhara (lecturing) kazi ya mwalimu ni kufundisha (teaching). Hizi ni taaluma mbili tofauti.Kama ni kuhodhi maarifa na unyanyasaji huo ni udhaifu wa mtu mmojammoja na ni udhaifu ambao hata baadhi ya walimu wanao. Hatuwezi kujumuisha (generalize) kwa mfano tukio la mwalimu mmoja kumbaka mwanafunzi kuwa in tabia ya walimu wote wanaume. Think criticall before you write.
 
Ninakusoma ndugu, suala kubwa hapa ni kuwa si kila mtu anaweza kuelekeza/kufundisha. Bila shaka ufundishaji ni taaluma na pengine si kila mtaaluma wa fani yoyote anaweza kuifundisha fani hiyo. Hili ndilo suala ninaloliangalia zaidi.
Wala hujagosea, ila kikubwa ni passmark yani GPA iliyosimama hayo mengine wengi wanaamini kwamba wahadhiri wata adapt na hali halisi, halafu kingine ni kwamba Mhadhiri ni tofauti na mwalimu wa shule ya msingi ama sekondari.

Tuchukulie mfano wa shule ya msingi, wanaofundishwa hapo ni watoto yani bado hawajajitambua, hawajui umuhimu wa elimu na pia wanahitaji wamezeshwe kila kitu, mwalimu anatafuna wao wameze yani wanarahisishiwa ili waelewe ulimwungu ni nini, elimu ni nini, manufaa ya elimu ni yapi, kwa kifupi hii elimu ya awali ni ya kumfanya mtoto ajitambue na pia kutambua namna ya kuishi katika mazingira husika.

Hii ni tofauti na chuo, chuo hapa unapewa kidogo sana mengine ujitafutie ili kuongeza uelewa zaidi katika hilo somo husika na ndio maana wahadhiri hawahitaji elimu ya saikolojia kukusoma wewe mwanafunzi hii huja automatically pale atakapofundisha kwa muda fulani.

Unayoyasema ni sawa pia sio mbaya wahadhiri wakapewa training ya saikolojia ili waweze kuwatambua wanafunzi wao haraka lakini waliopo vyuoni ni watu ambao wanajitambua tayari, ni watu wazima, wengi wao wanaumri wa kuanzia miaka 18 hivyo hakuna umuhimu wa kumbembeleza huyu asome maana tayari ni mtu mzima anajitambua.
 
Back
Top Bottom