Sidhani kama hiyo paper inadhihirisha ukilaza wa mhadhiri. FT 211 Principles of Food Processing and Preservation ni elective course inayotolewa kwa degree 3 (Agric. General, Human Nutrition na Family and consumer studies).
Hiyo ni Test1, ulitakiwa upitie test nyingine na final exam (end of semester examination) tuone zikoje. Kama Test ya kwanza labda mambo hayajaiva sana na mwalimu anafocus mainly kwenye factual information.
Maswali ya kujazia sioni kama ni tatizo hasa kama hatuna course objectives. Pia kuna issue ya ukubwa wa madarasa ambayo kwa sasa ina athiri vyuo vingi SUA ikiwemo na pia mwalimu ana masomo mangapi (teaching load) n.k. hivi vyote kwa kiasi fulani vinaweza vikapelekea maswali ya aina hiyo (kujazia na MCQ). Maswali aina hiyo pia hupatikana vyuo vingi duniani.
Tusisahau swala la course hii inafundishwa kwa undani kiasi gani ukichukulia kuwa wanafunzi wanao ichukua siyo wa food science and technology.
Hapa sina nia ya kutetea wahadhiri inawezekana kweli akawa kilaza-lakini evidence/ushahidi ulio toa haujitoshelezi kufikia msimamo uliochukua. Fanya uchunguzi zaidi kuhalalisha hitimisho lako.