Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 990
Nimekuwa nikisikia vijana wengi wanalalamikia kufelishwa masomo au kucheleweshwa kumaliza masomo (graduation) hata kama wamefanya vizuri. Ajabu haya matatizo yako katika vyuo vikuu maarufu hapa nchini vya University of Dar Es Salaam (UD) na Sokoine University (SUA). Mzumbe pia iliwahi kutokea hata mhadhiri mmoja akakamatwa kwa kumtongoza na kumtishia kumfelisha mwanafunzi wake wa kike wa uzaili (Masters degree). NAULIZA HII NI KUTOKUJUA KAZI ZAO HAWA WAHADHIRI?. Afrika kusini ilitokea mwanafunzi mmoja akichoka kuonewa aliamua kumpiga risasi mhadhiri. Na kenya pia matatizo kama haya tunayasikia. Najaribu kuwaza ama ni tatizo la wahadhiri na waalimu wasomi waswahili au wasimamizi katika vyuo hivi hawatimizi majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamia haki na sheria za vyuo. Mbona waswahili hawa katika vyuo vya nje hatujasikia wakionea wanafunzi? Kama mwanafunzi anajiandikisha katika chuo kusoma Masters ya miaka 2 kwanini msimamizi asiulizwe kwa kumchelewesha hadi akae miaka 3 na yeye akiwa ametimiza mahitaji (requirements)?. Nadhani ili kuweka weledi hasa katika vyuo vikuu tunahitaji tume ya vyuo vikuu ifanye utafiti kwa hili na kukemea vitendo hivi ambavyo vinaaibisha vyuo vyetu hasa wanapokuja kusoma wanafunzi toka nchi za nje na kukuta madudu haya. Waliosoma katika vyuo vikuu hivi vya UD na SUA niambieni kama ni majungu ama kweli? na kama ni kweli mimi mnisaidie kukusanya maoni yenu niyapeleke TCU rasmi kuwatyetea wasomi hawa wanaoonewa