Wahadhiri wa Tanzania hawajiamini au matatizo ya wasomi waswahili?

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
3,216
Reaction score
990
Nimekuwa nikisikia vijana wengi wanalalamikia kufelishwa masomo au kucheleweshwa kumaliza masomo (graduation) hata kama wamefanya vizuri. Ajabu haya matatizo yako katika vyuo vikuu maarufu hapa nchini vya University of Dar Es Salaam (UD) na Sokoine University (SUA). Mzumbe pia iliwahi kutokea hata mhadhiri mmoja akakamatwa kwa kumtongoza na kumtishia kumfelisha mwanafunzi wake wa kike wa uzaili (Masters degree). NAULIZA HII NI KUTOKUJUA KAZI ZAO HAWA WAHADHIRI?. Afrika kusini ilitokea mwanafunzi mmoja akichoka kuonewa aliamua kumpiga risasi mhadhiri. Na kenya pia matatizo kama haya tunayasikia. Najaribu kuwaza ama ni tatizo la wahadhiri na waalimu wasomi waswahili au wasimamizi katika vyuo hivi hawatimizi majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamia haki na sheria za vyuo. Mbona waswahili hawa katika vyuo vya nje hatujasikia wakionea wanafunzi? Kama mwanafunzi anajiandikisha katika chuo kusoma Masters ya miaka 2 kwanini msimamizi asiulizwe kwa kumchelewesha hadi akae miaka 3 na yeye akiwa ametimiza mahitaji (requirements)?. Nadhani ili kuweka weledi hasa katika vyuo vikuu tunahitaji tume ya vyuo vikuu ifanye utafiti kwa hili na kukemea vitendo hivi ambavyo vinaaibisha vyuo vyetu hasa wanapokuja kusoma wanafunzi toka nchi za nje na kukuta madudu haya. Waliosoma katika vyuo vikuu hivi vya UD na SUA niambieni kama ni majungu ama kweli? na kama ni kweli mimi mnisaidie kukusanya maoni yenu niyapeleke TCU rasmi kuwatyetea wasomi hawa wanaoonewa
 
Maisha magumu mpaka unajuta kusoma chuo kikuu make msuli utadhani kifo hakipo, assignment kila wakati, mbaya zaidi ukichelewa ingia class unakuta quiz tayari sio ilo tu ukiulizwa swali ukashindwa unaambiwa "utagraduate hapo baadae baadae sio mwaka lasimi wa kumaliza! nawasilisha ebu nkagonge msuli make kesho saa kumi na mbili na nusu nina test
 
Mkuu wee acha tu kuna wahadhiri wanafanya maisha kuwa magumu hadi basi, sitamsahau prof. Mshimba na prof. Kundael ni noma bana.
 
Lakini ulimwengu tunaouendea hii haikubaliki maana mtu anaweza kujichukulia sheria na akafanya mambo mabaya. Haki wanafunzi wapewe na walifeli pia wasibebwe eti kwasababu ya kulipa pesa au rushwa ya ngono
 
Ndo maana Mwenge university wanaondoa hizo kapi zenye roho mbaya na tabia za uzinzi,Sasa wanajaza Mapadre na Masister tu.Baada ya miaka 5 hakutakuwa na Mhadhiri ambaye sio Pandre au Sister.Nchi ngumu hii, Maisha magumu Shule nayo ngumu Da!
 
Nimekuwa nikisikia vijana wengi wanalalamikia kufelishwa masomo au kucheleweshwa kumaliza masomo (graduation) hata kama wamefanya vizuri. Ajabu haya matatizo yako katika vyuo vikuu maarufu hapa nchini vya University of Dar Es Salaam (UD) na Sokoine University (SUA). Mzumbe pia iliwahi kutokea hata mhadhiri mmoja akakamatwa kwa kumtongoza na kumtishia kumfelisha mwanafunzi wake wa kike wa uzaili (Masters degree). NAULIZA HII NI KUTOKUJUA KAZI ZAO HAWA WAHADHIRI?. Afrika kusini ilitokea mwanafunzi mmoja akichoka kuonewa aliamua kumpiga risasi mhadhiri. Na kenya pia matatizo kama haya tunayasikia. Najaribu kuwaza ama ni tatizo la wahadhiri na waalimu wasomi waswahili au wasimamizi katika vyuo hivi hawatimizi majukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamia haki na sheria za vyuo. Mbona waswahili hawa katika vyuo vya nje hatujasikia wakionea wanafunzi? Kama mwanafunzi anajiandikisha katika chuo kusoma Masters ya miaka 2 kwanini msimamizi asiulizwe kwa kumchelewesha hadi akae miaka 3 na yeye akiwa ametimiza mahitaji (requirements)?. Nadhani ili kuweka weledi hasa katika vyuo vikuu tunahitaji tume ya vyuo vikuu ifanye utafiti kwa hili na kukemea vitendo hivi ambavyo vinaaibisha vyuo vyetu hasa wanapokuja kusoma wanafunzi toka nchi za nje na kukuta madudu haya. Waliosoma katika vyuo vikuu hivi vya UD na SUA niambieni kama ni majungu ama kweli? na kama ni kweli mimi mnisaidie kukusanya maoni yenu niyapeleke TCU rasmi kuwatyetea wasomi hawa wanaoonewa

Nakubaliana nawe kuwa sometimes wanayafanya maisha kuwa magumu bila sababu, ni kweli lazima kuwe na heshima ya shule but sidhani kama kumtaka mwanafunzi kimapenzi ndo heshima ya shule au Kumchelewesha kumaliza dissertation ndio heshima ya shule. Mi nadhani kila mtu aki play part yake wala hakutakuwa na upuuzi wanaofanya walimu wa vyuo, tena sio UD pekee, kila sehemu, Hata Mzumbe bado ipo hiyo kitu, IFM pia, hata binafsi nako Tatizo, Tumaini Iringa, Ruco, KIU, Makumira nk nako hizo element bado zipo japo si kwa sana lakini bado zinaleta ukakasi. Hatusemi wanafunzi wapendelewe lakini kama mwalimu anatimiza majukumu yake na mwanafunzi akashindwa then hapo si tatizo lakini kwa sababu zisizo lazima kuziendekeza, tunaweza kuwa na jamii ya wasomi wanaosoma kwa kufuata wajibu wao ipasavyo bila misuguano na walimu. Kuna siku Mhadhiri atapigwa risasi huko tunakoelekea na tutaishia kuambiwa uchunguzi unaendelea.
 
Back
Top Bottom