Habari wana bodi, nimekuwa nikisoma baadhi ya articles zinazo ongelea mchango wa vyuo vikuu marekani katika uchumi wa taifa hilo especially kutengeneza innovators "silicon valley".
Kwa kiasi kikubwa maendeleo ya taifa la marekani yamechangiwa sana na innovations zinazofanywa na taasisi zake za elimu ya juu kama "think tank" ya nchi, kuanzia sera za uchumi, sera za mambo ya nje, etc.
Ukiangalia Taifa letu, wahadhiri wa vyuo vikuu ambao ndio wazalishaji wa wataalamu mbalimbali wamekuwa wakilipwa pesa kidogo sana ukilinganisha na wakurugenzi wa mashirika ya Umma au wabunge( ambao hawana mchango wa maana kwenye taifa hili uki compare na mchango unaotolewa na wahadhiri wa vyuo vikuu. Jiulize kibajaji au musukuma anawezaje kulipwa mshahara na marupurupu kuliko Prof au Dr, wa chuo kikuu?
Mimi ningemuomba Rais Samia waangalie hawa watu kama kweli tunataka hili taifa lisonge mbele. Licha ya kuongezewa mishahara serikali ipeleke pesa za kufanya tafiti mbalimbali na maamuzi ya wanasiasa yazingatie recommendations za wataalamu wetu.
Mtu ana PhD analipwa mshahara wa mil 3 au 4 na hapo bado makato kweli unategemea atakuwa na morale ya kufundisha? Au ndio atakuwa busy kufanya kazi zake za nje? Serikali inatakiwa kuona wapi inaweza kuwekeza pesa na zikawa na tija kwa taifa hili.