Wahadhiri wanastaafu miaka 65 waruhusiwe kuendelea kufundisha kutokana na Uhaba wao

Wahadhiri wanastaafu miaka 65 waruhusiwe kuendelea kufundisha kutokana na Uhaba wao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, ameisisitiza Wizara ya Elimu kuhakikisha wanaliangalia upya suala la Wahadhiri ili waweze kuendelea kufundisha hata baada ya kutimiza miaka 65, kwani wengi wao kwa umri huo ndiyo wanakuwa wamezidi kubobea kwenye taaluma zao.

Kauli hiyo ameitoa Bungeni leo Juni 14, 2021, mara baada ya kuibuka mjadala wa Wahadhiri hao kuendelea kufundisha kwa kuwa kuna uhaba mkubwa wa Wahadhiri nchini, swali ambalo liliulizwa na mbunge wa viti maalum Dkt. Thea Ntare, ambapo serikali ilisema kuwa itahakikisha inaangalia namna bora ya kurekebisha sheria hizo ili kuendana na uhitaji wa sasa wa soko la Wahadhiri nchini.

"Naibu Waziri hili mkalitazame kwa sababu mtu anapofikisha miaka 65 ndiyo amebobea kwenye eneo lake, sasa ukimuondoa huyo ukasema unatengeneza ajira mpya hakuna uhalisia, kwa sababu unayemuajiri haweza kuwa kama huyo mwenye miaka 65, kuna Maprofesa wengine hawana kazi za kufanya lakini wamestaafu na vichwa vyao viko sawa sawa wanaweza kuendelea kufanya kazi," amesema Dkt. Tulia

EATV
 
Yaani mtu uajiriwe kufundisha chuo ukiwa na miaka 25 au 30 then ufanye kazi hadi miaka 65 bado tu uwe na hamu ya kuendelea kufundisha.
Hao maprof waache tamaa, wawaachie wengine waimplement knowledge zao.
 
Graduates wapo wengi sana GPA 2.0. Vijana hawataki kusoma wanataka kuuza sura tu insta unategemea wahadhiri watapatikana vipi? Huku tunakoenda hata madaktari tutakuja kukosa unless tupanue magoli waingie mbumbumbu.
Kwahiyo hao wahadhiri hawafai, maana products zao ndio hizo GPA za 2.0.

Muhimu sasa wasife maana mwisho wa siku hizo GPA za 2.0 ndio zitakuja kufundisha.
 
Kwahiyo hao wahadhiri hawafai, maana products zao ndio hizo GPA za 2.0.

Muhimu sasa wasife maana mwisho wa siku hizo GPA za 2.0 ndio zitakuja kufundisha.
Unaweza kumpeleka punda mtoni, ila huwezi kumlazimiaha kunywa maji. Sio tu wahadhiri, hata madaktari, mainjinia, ma pilot nk itabidi waende vilaza.
 
Mbona mimi naona kustaafu raha sana!
Unless, labda hukujipanga. Na hilo silitegei kutoka kwa Wahadhiri
... inategemea unaliongelea jambo kwa angle ipi! Imagine kuna debate "kazi ya uhadhiri ni rahisi vs kazi ya uhadhiri ni ngumu"; wahadhiri wengi kama sio wote watakubaliana kwamba kazi yao ni ngumu sana! Ngumu sana maana yake inachosha sana akili na mwili so logically wangepaswa kupumzika/staafu mapema even at 55! Ila kwa kuwa hili lina maslahi kwao, watakwambia at 65 ndio kwanza akili inachanganya! Ha ha ha! Binadamu ni wanafiki sana.

Ni sawa na kazi ya siasa/urais; utaambiwa ni ngumu kuliko kazi zote duniani ila wanakimbilia kugombea at 70's ili wakafanye kazi ngumu kuliko walizostaafia at 50/60!
 
Haya mabunge mbona yana uhaba wa akili hivi... Bado yanaishi miaka 50 iliyopota.. ... rubbish
 
Kwa kauli hii ni kwamba yule "babu Profesa" anayefundisha kwa mkataba anazidi KUJIPAKULIA MINYAMA huku kijana mhitimu mwenye ka GPA kake kazuri akisubiri katika benchi.

Iko wapi "succession plan" katika taasisi za elimu kama Profesa mstaafu anakua ni mshindani wa nafasi ya ajira na kijana ambaye aliyakiwa kuajiriwa kama tutorial assistant ?
 
Ngumu sana maana yake inachosha sana akili na mwili so logically wangepaswa kupumzika/staafu mapema even at 55! Ila kwa kuwa hili lina maslahi kwao, watakwambia at 65 ndio kwanza akili inachanganya! Ha ha ha! Binadamu ni wanafiki sana.
Unasahau kuwa Brain na Physical body viko tofauti sana, unapofanya sana kazi za nguvu mwili unachoka zaidi unafika wakati unaweza kuumiza mwili wako lakini kwa kesi ya akili(brain) ni tofauti, kadiri unavyotumia ndivyo unavyokuwa kuwa mzuri zaidi.
 
Hivi inakuwaje maprofesa hawaandai wahadhiri wa kutosha? Shida complications nyingi sana. Wao wastaafu na kuondoka chuo muda ukifika. Hakuna cha nini wala cha nani....cha muhimu waandae vijana wa kutosha waache kufanya mambo magumu bila sababu.
 
Uyu nae akili zake fupi kuliko uhalisia wake kumbe kwaiyo sisi vijana tuendelee kuteseka huku na phd zetu hajambo nini huyu dada sijui mama
 
... inategemea unaliongelea jambo kwa angle ipi! Imagine kuna debate "kazi ya uhadhiri ni rahisi vs kazi ya uhadhiri ni ngumu"; wahadhiri wengi kama sio wote watakubaliana kwamba kazi yao ni ngumu sana! Ngumu sana maana yake inachosha sana akili na mwili so logically wangepaswa kupumzika/staafu mapema even at 55! Ila kwa kuwa hili lina maslahi kwao, watakwambia at 65 ndio kwanza akili inachanganya! Ha ha ha! Binadamu ni wanafiki sana.

Ni sawa na kazi ya siasa/urais; utaambiwa ni ngumu kuliko kazi zote duniani ila wanakimbilia kugombea at 70's ili wakafanye kazi ngumu kuliko walizostaafia at 50/60!
Nimekuelewa vizuri sana. You are very right! Kwa upande wa debate, ningekuwa upande wa " ni ngumu sana". Kustaafu at 60 years old, was extremely good for them.
 
Back
Top Bottom