GE2025 Wahadzabe wajipanga Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025

GE2025 Wahadzabe wajipanga Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jamii ya Wahdzabe wanaopatikana Eyasi, Karatu mkoani Arusha wamesema wapo tayari kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 ili kuchagua kiongozi atakayewatambua kama sehemu ya Watanzania.

Mmoja wa wanakabila hilo anayefahamika kwa jina la Dudukwe amesema: “Sisi kama Wahadzabe mwaka huu tunaenda kupiga kura, ninayo kadi ya kupiga kura, hata sasa hivi ipo mfukoni natembea nayo.”

Aidha, kiongozi wa eneo hilo, Felex Ebahati amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wakazi wa eneo hilo wanapata haki yao ya kupiga kura na kuchagua kiongozi wanaomtaka, huku akieleza mbinu ya kuwapata wote kwa pamoja ni kuwapatia chakula kutokana na kazi yao ya kujipatia chakula kwa uwindaji wa kila siku.

Hayo yamejiri leo Oktoba 1, 2025 baada ya TBC Digital kuitembelea jamii hiyo ya Wahadzabe kupata maoni yao kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
 
Wakapige tu maana wao barabara na shule sio mambo yao ya msingi
 
Nilijua tu hii taarifa imeletwa na Tbccm lichaneli la taifa linaloshabikia ccm kuliko hata Channel 10
 
Back
Top Bottom