Wahamiaji haramu tisa wa Kenya wakamatwa Dodoma Tanzania

Wahamiaji haramu tisa wa Kenya wakamatwa Dodoma Tanzania

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu wawili akiwamo Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kifaru Kelvini Mpoli (39)Mkazi wa Himo, Kilimanjaro, na Cathbert Kirita (58) Mkulima na Mkazi wa Kilema Moshi kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu 3 kutoka Kilimanjaro kwenda Songwe kupitia njia ya Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto, amesema mnamo tarehe 14/02/2020, walikamatwa huko katika kijiji Cha Mtera Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma, walikamatwa wahamiaji haramu watatu ambao ni raia wa Kenya wenye asili ya Somalia.

"Wahamiaji haramu hawa watatu walikamatwa katika kijiji Cha Mtera Wakiwa wanasafirishwa na watanzania, wahamiaji hawa Wakiwa ni raia wa Kenya wenye asili ya Somalia waliingia nchini bila vibali, Kati yao Wanawake wawili na Mwanamme mmoja walikamatwa wakisafirishwa kwenye gari namba T. 248 AWA, Nissan Patrol rangi nyekundu".

Aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni" Abdirahmani Mohamed (25), Luul Mohamed (30) na Hawa Gedow (18) wote Wakiwa ni Wasomali wenye uraia wa Nchini Kenya" amesema Kamanda Muroto.

Pia amesema mnamo tarehe 03/2/2020, katika kijiji Cha Chinene, Kata ya Haneti, Tarafa ya Itiso Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma, katika njia ya Dodoma- Arusha, walikamatwa wahamiaji haramu sita (6) raia wa Somalia waliokuwa kwenye gari la abiria lenye namba T.858 DAP Mali ya Kampuni ya Capricorn, kutoka Arusha kwenda Mbeya.

Amesema wote walikuwa na hati za kusafiria kutoka Kenya lakini walitiliwa mashaka na kubainika waliingia nchini bila uhalali watuhumiwa walifikishwa Mahakamani kwa kushirikiana na Idara ya uhamiaji mkoani Dodoma na kubainisha kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.

Pia kupitia oparation mbalimbali wameweza kukamata watuhumiwa watano kwa kosa la unyang'anyi wa pikipiki katika maeneo mbalimbali hapa Mkoani Dodoma.

" Mtandao huo umenaswa na watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na tunaendelea na Mahojiano zaidi kupata mali zilizoibiwa na washiriki wengine" amesema Kamanda Muroto.

Ametoa wito kwa watanzania kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili kuweza kusafisha tatizo la uharifu hapa Dodoma na nchi kwa ujumla, pia amewataka wananchi ambao wameibiwa vitu vyao kufika katika kituo Cha Polisi kutambua mali zao wakiwa na vithibitisho vya kumiliki Mali hizo.
 
hongera sana vyombo vya dola mazee..mengine ni mashababi tu, mbona hayana hati za usafiri!
 
Nchi hii mtu akipita nchini (on transit) ni muhamiaji haramu, let be serious asee..!
Hii habari inaukakasi,kwanza Wakenya hawalipi viza kuingia Tanzania so wanakwenda boda wanagongewa free na kuingia Tanzania,labda kama wali over stay na yenyewe ni kesi nyingine
 
Walimu wawili wa shule ya sekondari Kifaru wawekwa korokoroni kwa kosa kujihusisha kuwahifadhi na kuwasafirisha wahamiaji haramu kutoka Kenya waliokuwa safarini kwenda Zambia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kamanda Gilles Muroto alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakitumia gari aina ya Nissan Patrol likiendeshwa na mmoja wao kati ya hao walimu kutoka Arusha kwenda Mbeya kisha kuingia Zambia kwa njia za panya.

Tatizo nini walimu wetu mpaka kuwa mawakala wa wahamiaji haramu..?
 
Jana nilienda kusafisha picha niliona akina dada wamevaa vizur wanaongea lugha siilew nikama kisomali iv nilipo wauliza kua nyie ni wasomal aise walisepa fasta
 
Sasa kama walikuwa wahamiaji haramu,kwanini wasafilishe tena? Labda ungesema wasafili au wapitaji haramu.
 
Bila kufanya hivyo watapata wapi pesa ya kuhonga?
Au mnataka wafe kwa nyegezi?
Waoneeni huruma nao ni binadamu!
 
Back
Top Bottom