Wahandisi watatu kusomewa hati mpya ya uhujumu uchumi, Septemba 30, 2025

Wahandisi watatu kusomewa hati mpya ya uhujumu uchumi, Septemba 30, 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Wahandisi watatu na muongoza watalii mmoja wanaotuhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi wanatarajia kusomewa hati mpya ya mshataka ya uhujumu uchumi Septemba 30, 2025.

Wahandisi hao ni Faustine Malya (44) mkazi wa Salasala, Emiliani Kimaro (35) mkazi wa Kibaha, Nelson Jacob (32) mkazi wa Kimara Mwisho (wahandisi) na muongoza watalii Tumaini Mollel (30) mkazi wa mkoani Mwanza, Kiseke.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa walijipatia zaidi ya sh milioni 300 kutoka Shirika la Nyumba la taifa Tawi la Mtwara, Halmashauri ya Jiji la Tanga, Skyline Properties Ltd, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kampuni ya mafuta ya Camel.

Wakili wa Serikali Burton Mayage alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Amos Rweikiza wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salaam kuwa kulikuwa na amri ya kubadilisha hati ya mashtaka kama ambavyo waliomba.

Hata hivyo, mawakili wa washtakiwa hao Peter Shapa na Pharis Mshana hawakuwa na pingamizi, lakini mshtakiwa wa kwanza Malya ambae hana wakili aliomba muda kidogo kwa sababu wana wagonjwa nyumbani wanawahudumia.

Hakimu Rweikiza alisema ni suala la wao kusomewa tu mashtaka, kwa hiyo Kesi imeahirishwa hadi Septemba 30,2025 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa hati mpya.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa walijipatia fedha hizo kutoka kwenye miradi inayosimamiwa na kampuni ya Sec East African Ltd inayohusiana na masuala ya kufunga lifti katika majengo mbalimbali, baada ya kubadilisha akaunti namba za kampuni hiyo na kuweka namba zao za akaunti za benki.

Ilidaiwa kuwa walifanikiwa kufanya hivyo, baada ya kughushi sahihi ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Tian Chun, sahihi ya Mkurugenzi wa Masoko Ntuli Mwankusye na sahihi ya mhasibu Gabriel Makundi.

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa hayo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kughushi kati ya Novemba 5, 2021 hadi Aprili 14, 2023 ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

 
Wanawaagiza wao wakigundulika wanawaangushia jumba bovu, nimeelewa bila shaka...
 
washtakiwa walijipatia zaidi ya sh milioni 300 kutoka Shirika la Nyumba la taifa Tawi la Mtwara
Yaani 300m tu? Watoto wa DG-EYS-S wamapiga picha na dola laki 3 sawa na milioni 800 lakini hawaulizwi wamepata wapi....Wanatembelea magari ya bilioni 10 sirikali ipo kimya.
 
Back
Top Bottom