Prezdaa Shaco
Member
- Sep 3, 2013
- 46
- 8
Chuo kuzuia matokeo ya mwanafunzi anaedaiwa ni upungufu wa fikra kwa wasomi wetu wanaofanya kazi kwa mazoea tuu, mwanafunzi yupo mwaka wa 1au 2 unamzuilia matokeo ili iweje wakati bado yupo chuoni na mnaweza kumbana wakati wowote sasa mtu asoma mfano muce then kwao bukoba hujamuonyesha matokeo yake akajua kama kuna somo amesap au vipi unategemea ataweza kutoka bukoba akafatilie matokeo chuoni?? Mimi sioni busara za wasomi hapa zaidi ya kuturithisha chuki na roho mbaya tutakayoenda lipiza kisasi makazini na uraiani... Hivi kweli huu ndio uzalendo tunaofundishwa tuwe nao wasomi...!!?? Imeniuma sana raisi wa muce (daruso)amepigiwa simu kuulizwa na kujibu kuwa ni jambo ambalo kashindwa kulipigania; kwa nini asijiuzulu kuonyesha hisia za wanyonge anaowawakilisha?? Au mnaendelea kutetea msemo wa aliye shiba hamjui mwenye njaa?? Hii nchi inaenda wapi?? Nyinyi wasomi mliounda sheria za kuzuia matokeo hamkusoma bure nyinyi enzi za mwalimu?? Hivi uzalendo unajengwa jkt kwa kufanyishwa kazi ngumu na njaa au unajengwa kwa elimu huru na isio na ubaguzi kwa raia wake...? Imeniuma sana tunajenga taifa linaloelekea wapi