Wahaya punguzeni mbembwe

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
8,447
Reaction score
19,425
Habari wana jukwaa.

Kama kawaida ni jumapili tulivu nimepumzika naangalia Tv naona kuna tukio linaendelea Ikulu la mabalozi wa Marekani na Vietnam wanajitambulisha.

Sasa katika kujua hili na hili kuhusu hili tukio na uhusiano wa Tanzania na mataifa hayo mawili naona mtangazaji Emmanuel Buhohela anamuhoji balozi Wilson Masilingi.

Mzee ana mbwembwe nyingi sana na ananiacha hoi anavotumia neno Korobao aki refer Barakoa.Kinacho nichosha kuhusu huyu muhaya ni pale akirekebishwa na mwandishi kuwa sio Korobao ni barakoa yeye anajitetea kuwa asamehewe maana yeye amezoea sana lugha za kimataifa.

Sasa jamani ni lugha gani ya kimataifa ukiizoea barakoa unaiita korobao maana lugha ya kimataifa wengi tunayoitumia na kuizoea ni kiingereza ambacho kwao barakoa ni mask. Nashindwa kuelewa kwanini asikubali kwamba hawezi kulitamka neno husika kwa ufasaha kuliko kutuzuga.

Wahaya punguzeni mikwara
 
Kama ingekuwa Masilingi sio muhaya ungesemaje! Alafu tusikariri ni tabia ya mtu mwenyewe tuache kusingizia makabila mambo ya zamani hayo.
 
kila kabila lina kasumba zake na kasumba hizi huiathiri jamii husika sehem kubwa japo si yote, hii kasumba ya kupenda sifa na kujimwambafy wahaya wanayo sana mkuu hivo tpo sahih
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…