appoh
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 5,262
- 2,184
MAMBO YA WANASHERIA:
Baada ya kumaliza Degree yake ya Sheria, Bwana Rwegashora aliamua
kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufung ua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake, alimwona dada mmoja mtanashati
na mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi
Ndipo akanyanyua mkoni wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizungusha kwenye kiti cha kuzunguka.
Wakati dada alipokaribia, Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana
alijifanya yupo busy na kuongea na simu muhimu.
Wakati anaongea na simu, alisikika akisema: No, No, No ..., absolutely No.
Wajulishe hao lay persons wa New York kuwa siwezi kushughulikia kesi ambayo itanilipa chini ya Shs 50 million. Mimi ni profesional lawyer and I'm crossing the border to serve international community.
Aka-pose kidogo na akanywa maji, kisha akaendelea.....
Naweza kuanza kukusanya primary evidence next week, but tell them watume kwanza ten million kwa kuanzia...
Hahahahaha you don't know my Account Number, Mr Roger? Ok, waambie watume kwenye Account ile ile waliyonitumia million 100 last month...
Aka-pose tena akimeza fundo la maji na kurekebisha tai yake, kisha akaendelea...Ok usisahau kumueleza Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Marekani kuwa nitakuja New York mwezi ujao, maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu Mholanzi, kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza
Wakati anaongea hayo yote, yule dada alikuwa ametulia na anamwangalia Bwana Rwegashora anavyojizungusha kwenye kiti chake na kujinasibu huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL.
Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu ya TTCL chini, kisha akamgeukia dada mrembo. Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana, kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana, ninapokea simu nyingi sana mpaka nimechoka. Simu nyingi ni za wateja wa nje ya nchi.
Anyway nikusaidie nini?
Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopita. ahahaha najua utatamani kuiona sura
ya Bwana Rwegashora ilikuaje.