Wahaya wanasema bei ya senene imeporomoka kiasi cha wawindaji kupata hasara!

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Habari kutoka mkoani kagera zinasema bei ya senene imeporomoka sana msimu huu, mpaka sasa hawaelewi kama mporomoko huu umetokana na bei ya senene kwenye soko la dunia. Habari za uhakika zinasema bei ya senene kwa sasa inampa hasara wawindaji wanaowinda na kukatamata senene hawa na wanaomba kutazamwa kwa jicho la huruma ikiwezekana wapate bei elekezi.


raw senene



semi - processed senene



processed senene
 
Hakuna kitu kama hicho,Kama ni utani peleka jukwaa la jokes

Senene waliojazwa kikombe cha chai cha plastiki(waliotolewa maganda) sh elfu 3,000-5,000.

Hiyo bei ya kila msimu.
 
Huku kwetu sato hazishkiki tunaishia kula kambale tu,yaani kila kukicha ni bora ya jana[emoji1321]‍♂️
 
Hakuna kitu kama hicho,Kama ni utani peleka jukwaa la jokes

Senene waliojazwa kikombe cha chai cha plastiki(waliotolewa maganda) sh elfu 3,000-5,000.

Hiyo bei ya kila msimu.

wanasema senene ni fursa nzuri sana ya uwekezaji ikichukuliwa kwamba senene anaweza kutumika kama "snack" akatafunwa mda wowote au akatumika kama mboga kwenye chakula.

wanasema matumizi haya yanachagizwa na ladha ati iliyoko kwenye wadudu hao ingawa wao wamenikatalia kuwaita wadudu ingawa nikiwauliza wako kundi gani la viumbe hai wanasema huko tusiende kwenye kwenye makundi ya biolojia maana ukisha muweka kwenye kundi la wadudu tu inaleta ukakasi kwenye ubongo na mtu anapotafuna hawezi kupata ladha yake.

wanasema ukitumia njia za kizamani garama ya kuwinda na kukama kikombe kimoja na alafu uwaprocess kuwaondolea makapi, wanasema 3000 - mpaka 5000 kwa kikombe ni ndogo sana.

wakaniambia ili ukamate wengi unahitaji kuweka mitambo ya kisasa lakini bado tatizo liko kwenye uondoaji wa makapi.

Hivyo wakasema biashara ya senene ni labour intensive business inayohitaji watu wengi, wakasema hivi mtu mmoja akikaa kumenya kwa siku atamenya kiasi gani?

sasa fikiri kama hawa wamenyaji ni watu wanalipwa mishahara, hebu anzia kwenye gharama za uwekezaji kukamata, kumenya, kuwaprocess, kuwafanyia packaging mwisho wa siku wamenyaji wanabaki watu kuwa ni watu wa kujitolea au kutumikishwa bila malipo.

Huu ni wakati ambapo kila mtu anatakiwa ale kwenye kazi anayoifanya sio huyu akimenya senene amenye bure na abaki ombaomba huku wengine wakifanya shughuli nyingine wanalipwa na kuendesha maisha yao.

Ki msingi mimi nimewaelewa ila kuelewa kwangu na kutokuelewa kwangu hakuna tofauti kwao ila nikawaambia msaada wangu unaweza kuwa kupiga yowe ili wale ambao kuelewa kwao na kutokuelewa kuna tofauti tuone kama watasikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…