Hakuna kitu kama hicho,Kama ni utani peleka jukwaa la jokes
Senene waliojazwa kikombe cha chai cha plastiki(waliotolewa maganda) sh elfu 3,000-5,000.
Hiyo bei ya kila msimu.
wanasema senene ni fursa nzuri sana ya uwekezaji ikichukuliwa kwamba senene anaweza kutumika kama "snack" akatafunwa mda wowote au akatumika kama mboga kwenye chakula.
wanasema matumizi haya yanachagizwa na ladha ati iliyoko kwenye wadudu hao ingawa wao wamenikatalia kuwaita wadudu ingawa nikiwauliza wako kundi gani la viumbe hai wanasema huko tusiende kwenye kwenye makundi ya biolojia maana ukisha muweka kwenye kundi la wadudu tu inaleta ukakasi kwenye ubongo na mtu anapotafuna hawezi kupata ladha yake.
wanasema ukitumia njia za kizamani garama ya kuwinda na kukama kikombe kimoja na alafu uwaprocess kuwaondolea makapi, wanasema 3000 - mpaka 5000 kwa kikombe ni ndogo sana.
wakaniambia ili ukamate wengi unahitaji kuweka mitambo ya kisasa lakini bado tatizo liko kwenye uondoaji wa makapi.
Hivyo wakasema biashara ya senene ni labour intensive business inayohitaji watu wengi, wakasema hivi mtu mmoja akikaa kumenya kwa siku atamenya kiasi gani?
sasa fikiri kama hawa wamenyaji ni watu wanalipwa mishahara, hebu anzia kwenye gharama za uwekezaji kukamata, kumenya, kuwaprocess, kuwafanyia packaging mwisho wa siku wamenyaji wanabaki watu kuwa ni watu wa kujitolea au kutumikishwa bila malipo.
Huu ni wakati ambapo kila mtu anatakiwa ale kwenye kazi anayoifanya sio huyu akimenya senene amenye bure na abaki ombaomba huku wengine wakifanya shughuli nyingine wanalipwa na kuendesha maisha yao.
Ki msingi mimi nimewaelewa ila kuelewa kwangu na kutokuelewa kwangu hakuna tofauti kwao ila nikawaambia msaada wangu unaweza kuwa kupiga yowe ili wale ambao kuelewa kwao na kutokuelewa kuna tofauti tuone kama watasikia.