Wahenga, munakumbuka 'gari la wanyonya damu'?

Wahenga, munakumbuka 'gari la wanyonya damu'?

KUDOLE CHA MWISHO

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2017
Posts
407
Reaction score
892
Habari wanazengwe!

Hebu tukumbushane hii habari ya miaka hiyooo.

HIVI KWELI GARI LA NYONYA DAMU NI KWELI YALIKUWA YANAKUJA MASHULENI?

Nakumbuka siku moja nikiwa darasa la tatu mwaka 1994 kuna mwanafunzi alingiaa darasani ghafla na kusema "gari la wanyonya damu linakuja" ndani ya sekunde 10 tu darasa zima likuwa tupu nimebaki peke yangu, na mimi mwenyewe nikatoka nduki hapo hapo.

Miaka hiyo kulikuwa sana na habari ya watu waliokuwa wanakuja na gari mashuleni kuja kunyonya damu kinguvu wanafunzi tena wanasemekana walikuwa na vioo hivyo ukiviangalia tu vinakuvuta unaenda mwenyewe na wanakunyonya damu mpaka unakufa. Habari hizi azikuwa tu shuleni kwetu bali shule mbalimbali za hapa Dar es Salaam na za mikoani wanafunzi walikuwa wakiamni hivyo.

Mpaka namaliza darasa la saba matukio ya wanafunzi kukimbia shuleni kuohifia kuwa kuna gari la nyonya damu yalikuwa yakijurudirudi lakini mimi hata siku moja sikuwahi kuona hao watu au hilo gari.

Siku hizi mashuleni sisikii tena habari za gari la nyonya damu kama enzi zetu. Kitu kinachonipa maswali kama ni kweli kulikuwaga na gari la nyonya damu au ilikuwa stori tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha shuleni kwangu chikongola, na ilikua tukikimbia waalimu wala hawatuzuii wala kutuadhibu kesho yako kitu ambacho hata mimi bado kinaniacha na maswali.
 
Dah, miaka ileeee! Hahahaha siku hizi kuna "Noah Nyeusi"! Yaani ilikua nikienda uzaramoni na gari INA tinted acha kabisa Wazaramo wanatoka nduki....hawataki uwape hata lift

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa ni kutishana tu, na uchache wa magari kila aliyemiliki gari aliitwa mnyonya damu. Hata siku hizi hizo kasumba bado zinaendelea japo ni tofauti na unyonya damu. Kipindi hiki mtu akipata utajiri kwa haraka utasikia ni Freemason, kumbe haina uhalisia, hiyo dhana inaenda ikipungua kwa ajili ya UTANDAWAZI.
 
😂😂😂 Nakumbuka nipo BUKOBA shule ya msingi, kila likipita gari jekundu basi ndukii na kujificha kwenye majani. Enzi hizo bana
 
Hii kitu nadhani ilikuwa Tanzania nzima, story za wanyonya damu zilifanya watu watembee barabarani kwa wasiwasi.
 
Back
Top Bottom