Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Pia aliwahi kuwepo mkali wao aliitwa SP..huyu bana alikuwa na sifa ya kuwatoa mabaka mabaka ka mjeda wale wote wenye allergy na sulphur.

Niliwahi kuinywa hii ikanibabua kifua nikawa natoka magamba ka kenge...

Kwakweli Mungu alitunusuru tu.
 
Dawa ili nifanya mpaka leo naogopa kunywa dawa .Na kupenda kuchokwa sindano hadi leo hii
 
Duh huyo mtu kama yupo mwambie aagize kinywaji chochote nitalipa. Nimemvulia kofia
 
Hizi dawa zilikuwa zinanionea kwenye kuniwasha,sitakagi hata kukumbuka.Usiku mmoja kulikuwa na mvua usiku mm nawashwa,mtu pekee aliyekuwa akinifariji ni marehemu mama lkn nayeye alifika wakati akachochoka akalala,sitasahau usiku ule ,ilikuwa mrefu ka mwezi mzima vile.Mwishoni hapa ndo tuligundua unameza piriton nusu saa kabla hujazimeza hapo huwashwi.Cloroquen ww Mungu anakuona.
 
Hiyo dawa hafai dadeki sitasahau, ilitaka kumtoa mama yangu uhai hiyo sio dawa ni poison wallah
 
Na kuna dada mmoja alitumia hizo dawa mpaka leo kuongea ni tabu
 
Niliwahi ku-over dose, nilwashwa na jasho adi godoro lililowa. Usiku ulikuwa mrefu asubuhi nilipewa maziwa nikatapika ndio nzima. Kilichofata drip za kutosha
 
Dawa hizo nmezitupa sn bora ilikuwa nichomwe sindano
 
Sijawahi kunywa hii dawa japo ni mhenga
 
Zimenitesa sana hizi kitu. Zilikua zinanifanya kama njuka wake...
 
Kuna dawa ya malaria ya sindano, iliyofuatia Chloroquine, ikiitwa "Christapen". Hii ilikuwa mbaya zaidi manake ukidungwa hiyo sindano lazima mguu ufe ganzi!
Dah ile sio gani sijui ni kitu gani manake kama umesimama utakaa mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…