Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

nakumbuka baada ya serikali kusitisha usambazaji wa chloroquine, waka-introduce dawa tiba nyingine ya malaria iliyoitwa fansida, ilikuwa ina nguvu sana.

kuna mwaka fansida ilitaka kuniua mazima huku najiona....iliniongezea homa maradufu.
 
[emoji16][emoji16][emoji16],ebana nilikuaga naiweka katikati ya ndizi au tonge ndo naimeza kukwepa uchungu.
Halafu ilikuwa nawshwa muda wa siku nne, ole wako uoge ,utajuta [emoji16][emoji16][emoji16]
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji106]-[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106],kweli we muhenga, mjomba umenielezea maswaibu yaliokua yakinipata
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji106]-[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106],kweli we muhenga, mjomba umenielezea maswaibu yaliokua yakinipata
Ha ha haaaa, dunia hadi kufika hapa ilipo wahenga tumelipa big price. Siku hizi wanakunywa dawa utadhani labda unakunywa chaki.
 
Ha ha haaaa, dunia hadi kufika hapa ilipo wahenga tumelipa big price. Siku hizi wanakunywa dawa utadhani labda unakunywa chaki.
Ngoma mchana inatulia kidogo, ebana jioni ikianza kuingia mawazo tele, huzuni
 
vijana waliozaliwa wakati mzee mwinyi anakaribia kumaliza mda wake wa urais, hawawezi kutuelewa haya tunayojadili hapa kuhusu klorokwini (chloroquine).

uhenga una gharama zake...acheni tu jamani.
Teh nashangaa hapa watu wamezaliwa enzi za mkapa ila wanavyochangia utasema walikuwepo
 
klorokwini ni kitu ingine nilimeza mara moja tu maishani miaka ya 99 au 2000 lakin cjasahau uchunguzi
 
Mie zilikuwa hazinipi shida, tatizo muda wa kumeza ule uchungu jamani mpaka kikombe nitakachotumia nitamaliza hata mwezi sikigusi, ila siwashwi wala kutapika ni kupona tu, ila uchungu ule niliziacha na kuanza kumeza fansida za Kenya rangi ya blue bahari
 
Aisee

Hazikuwahi kunisumbua

Kwangu ndio zilikuwa dawa bora kabisa za malaria
 
Iyo dawa imeniletea ulemavu wa kudumu kila nimalizapo kuoga lazima mwili uwashe. .hakika klorokwini sitakusahau
 
Ule muda wa kuwashwa ulikua ukifika, nazunguka nyuma ya nyumba naanza kujisugua kwenye ukuta zile kuta za upele zile nikitoka hapo mambo yanakua muswano kabisa.

Ila zilinikosakosa kuniondoa baada ya kubugi dose. Hazifai zile hata kidogo.
 
Mhenga mwenye mafanikio aliyewawahi kukutana ana kwa ana na chloroquine hospitali.
 
Bora harufu....kuwashwa jamani, nilikuwa nawashwa iwe ni sindano yake iwe ni vidonge.....lol!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…