Niko darasa la 5 nilikosea dose, ile 4x4x2, basi nikanywa asubuhi, mchana na ucku jamani asikuambie mtu. Usifanye mchezo roho inapotaka kuacha mwili, Kaka yangu ananiuliza dawa zako ziko wapi? Nikamjibu nimemaliza, wewe alikoroga mavi ya ng'ombe nadhani alichanganya na ya watu, nyie msisikie habari ya kufa.
Huku nje watu kilio, wanajua siamki, nikapewa maziwa fresh lita 4, nikanyweshwa na hivyo vinyesi, jamani Mungu yupo, akisema hufi hufi. Nilianza kutapika nilitapika mpaka nilikuwa siwezi kufumbua macho, kwa kifupi kila mtu alijua tu hell!! Mpaka ucku wa saa 4, ndio naenda kulala. Jinsi walivyonitandikia unajua kabisa wananiaga, niliogoshwe nikavalishwa nguo nzuri sana za kwangu kwa akili ya kawaida nilijua wananizuia na hii baridi ninayohisi. Kumbe wenzangu walikuwa wananiaga kuwa hakuna namna. Amini maneno yangu, usiku kama wa saa 7 ninaona kwa macho yangu malaika, mkononi kashika kitu kinatoa damu. Naona kwa macho yangu, akaingiza ule mkono wake tumboni kwangu, akatoa kitu nikahisi maumivu sana, akaweka kile kingine, naona kwa macho. Kushoto kwangu wamelala watu wengi, ambao walikuwa wako tayari ninapokata roho wanisaidie. Lakini wenyewe hawamuoni yule malaika, alipokuwa anaondoka nilipiga kelele kubwa sana, nikagongwa na kitu usoni kwa kishindo kikubwa sana. Niliona nyota kama 200 hivi, jasho lililowesha kitanda chote pamoja na nguo zote. Wakaniamsha wakasikitika sana, nikanywa maji nikalala mpaka kesho yake. Acheni jamani Mungu yupo.