Wahenga tukutane hapa

Wahenga tukutane hapa

-Awafu mwenye nguvu
-Pamela na kipini
-Siku ya gulio
-Tola alia gizani
-Watoto wageuka mawe
-Mkutano wa wanyama
-Nani atamfunga paka kengere
-Muwa uliozamisha meli
-Sadiki na Chitemo
-Jogoo wa ajabu
-Mpapai na mtete
-Kuku na yai
-Pepe mwanangu huna masikio
-Chopeko na mnofu.
 
Huyo sikiri sijamsoma mkuu.

Nazikumbuka tu hizi.

-Jogoo wa ajabu
-siku ya gulio katerero
-chitemo na sadiki
-Karudi baba mmoja
-sungura mjanja
-
"Sungura mjanja,"

Sisi wa zamani kidogo tulisoma Sungura na fisi (cha wageni na cha wote) na sizitaki mbichi hizi.

Hizi story zote zilikuwa zinaongelea ujanja wa sungura
 
-Awafu mwenye nguvu
-Pamela na kipini
-Siku ya gulio
-Tola alia gizani
-Watoto wageuka mawe
-Mkutano wa wanyama
-Nani atamfunga paka kengere
-Muwa uliozamisha meli
-Sadiki na Chitemo
-Jogoo wa ajabu
-Mpapai na mtete
-Kuku na yai
-Pepe mwanangu huna masikio
-Chopeko na mnofu.

Mkuu hapa umechanganya vitabu vya zamani kidogo na vilivyokuja kufanyiwa marekebisho kati ya 1995-1997. Kama hiyo sadiki na chitemo kabla ya hapo ilikuwa sadiki na sikiri, Ushairi wa Kuku na yai nao ulianza kutumika kwenye mabadiliko hayo ambapo darasa la tano ulikwa kwenye mfumo wa swali na darasa la sita ukiwa kwenye mfumo wa majibu. Muwa uliozamisha meli nayo ilikuja kwenye marekebisho hayo
 
Kalumekenge alikataa kwenda shule, ikatafutwa fimbo impige Kalumekenge aliyekataa kwenda shule, fimbo ikagoma. Ukatafutwa moto uunguze fimbo iliyokataa kumpiga Kalumekenge aliye......!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wengine humu hamkuikuta ile ya mchezo wa kibaba-baba/kimama-mama, halafu wakati wa kufanya tunafanya kinguonguo aka kiuongo-uongo..... ...kimbembe chake mkikamatwa ni fimbo na vifinyo kwenda mbele..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wengine humu hamkuikuta ile ya mchezo wa kibaba-baba/kimama-mama, halafu wakati wa kufanya tunafanya kinguonguo aka kiuongo-uongo..... ...kimbembe chake mkikamatwa ni fimbo na vifinyo kwenda mbele..

Sent using Jamii Forums mobile app
Teh teh teh...baadhi yao wale wakubwa walikua wakichaguana kumbe walikua wanaangalia mbali zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karudi baba mmoja,toka safari ya mbali.
Kavimba yote mapaja,na kutetemeka mwili.
Watoto wake wakaja,ili kumtaka hali.
Wakataka na kauli iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa ninaumwa kwelikweli.
Roho naona yachinjwa,kifo kinanikabili.



Sent using Jamii Forums mobile app
Ubeti wapili hujamaliza
Akatamka mgonjwa,Ninaumwa kwelikweli,
Hata Kama nikichanjwa,Haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,kifo kimenikabili,
Kama mnataka Mali,mtaipata shambani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakazidi kumchimba baba mwenye homa kali
Baba yetu watufumba hatujui fumbo hili
Akili yetu nyembamba haijajua methali
Sema iko wapi mali itufae maishani.
Urithi tunatamani,Mali yetu ya halalali




Madogo walikomaa hao.[emoji23][emoji23][emoji23]
Ubeti wapili hujamaliza
Akatamka mgonjwa,Ninaumwa kwelikweli,
Hata Kama nikichanjwa,Haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,kifo kimenikabili,
Kama mnataka Mali,mtaipata shambani.

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakazidi kumchimba baba mwenye homa kali
Baba yetu watufumba hatujui fumbo hili
Akili yetu nyembamba haijajua methali
Sema iko wapi mali itufae maishani.
Urithi tunatamani,Mali yetu ya halalali




Madogo walikomaa hao.[emoji23][emoji23][emoji23]


Sent using Jamii Forums mobile app
Baba aliye kufani,akajibu Lile swali,
Ninakufa masikini,baba yenu Sina Hali,
Neno moja lishikeni,Kama mnataka Mali,
Kama mnataka Mali,mtaipata shambani.

[emoji4][emoji4][emoji4][emoji2960],Kaz kwako kaka,,tuendelee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom