Wahenga, tuwakumbuke watangazaji wetu RTD

"Hii ni taarifa ya habari kutoka radio Tanzania Dare Salam....msomaji ni Mimi Bujaga Izengo Kadago". Nilikuwa naipenda sana sauti yake ya mapozi sijui Yuko wapi huyu .
 
Selemani kumchaya umemrudia mara mbili, nafasi moja muweke Agoro Anduru External Service. Jamaa alikuwa akiandika habari haipiti kwa Mhariri inaenda moja kwa moja News room kutokana na command yake ya Oxford English. Akiwa Musoma Alliance Secondary rekodi yake ya somo la English haijavunjwa hadi leo. Ameacha vitabu kadhaa. Balozi Osoro Opanga (Mkuu wa Itifaki mstaafu) ambaye alikuwa Msaidizi wa Mwl kwenye ukalimani wa lugha (anaongea na kuandika lugha 21) alimvulia kofia Agoro Anduru kwenye Kiingereza.
 
Umesahau Masoud Masoud, Amina Mollel (MP) na yule mwingine wa Dodoma aliyekuja kuwa mbunge na N/Waziri Habari na Michezo.
 
Ezekiel Malongo - Michezo
 
Umewakumbuka wengi sana..kuna hiki kipindi cha "tunawaletea mazungumzo baada ya habari" pia kuna kipindi cha "harakati" na kipindi cha "club raha raha leo show"
 
"Hii ni taarifa ya habari kutoka radio Tanzania Dare Salam....msomaji ni Mimi Bujaga Izengo Kadago". Nilikuwa naipenda sana sauti yake ya mapozi sijui Yuko wapi huyu .
Hivi Marine Hassan Marine angelikuwa hai leo Charles Hilary angeenda Ikulu Znz kweli?
 
Ingekua nafac yake ile
Umeona eee....

Jamaa alikuwa mjenzi hodari wa Kiswahili kwa kubuni misamiati, nahau na misemo mipya.

Aliweza kutumia tajiriba na ragba yake kuuza sera ya serikali ambayo haiuziki (iliyokwama).

Nyumbani kwangu sauti yake iliposikika tu watu wazima kwa wadogo walichomoka vyumbani na jikoni kuja kubanana kwenye makochi kumuona na kumsikiliza MARINE HASSAN MARINE.

Naamini hata BBC, DW, VOA wangetoa donge nono kiasi gani Dr. Magufuli, Dr. Mwakyembe na Dr. Rioba wasingemuachilia.

R.I.P. Mzee wa TBC ARIDHIO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…