Waheshimiwa wana JF - Hongereni!

Waheshimiwa wana JF - Hongereni!

Status
Not open for further replies.
Sawa basi...uliyoyaandika nimeyasoma...

Mimi naona kupata umaarufu hapa JF ni kuuandika hoja maarufu na sio kupingana na mtu anayeleta hoja maarufu hapa JF ili watu wakuone kuwa unaweza kupingana naye tu pasipo sababu muhimu. Ina silitisha wakati tunajaribu kuwarekebisha wageni waliokuja na kasi ya kutetea mafisadi hapa JF tunagundua kuwa wameshaaambukiza na wazoefu
 
Unaona sasa...tatizo humu kuna mijitu inajiona yenyewe ndiyo yenyewe...eti ina akili sana kushinda wengine....na mawazo yao kila siku ndio bora!! Kila siku inashindana hapa kuonyesha imesomea nini hata kama haijasomea hivyo vitu. Hii tabia ni mbaya sana na inapofikia jitu kujiona lenyewe ndio lina akili kushinda wengine basi ujue ni tupu na ili kujilazimisha kuamini kwamba lina akili inabidi liwa-put down wengine.

This is not directed at any one in particular but if the shoe fits then you know what time it is....

Hiki kiatu naona kimenifit sawasawa! Nadhani yote haya ni katika kujaribu kuwekana sawa. It is all good.
 
"Mkjj hebu timiza usemi wako huu"
Kumbukeni yanaanzia JF yanaisha kwenye vyombo vyetu vya habari kama itakavyokuwa kesho kwenye moja ya magazeti! Wajumbe Butiama kaeni chonjo...


na Happiness Katabazi (Tanzania Daima)



TUHUMA za ufisadi zilizosambazwa katika mtandao wa intaneti zikimlenga Spika wa Bunge, Samuel Sitta, zimesababisha Ofisi ya Bunge kuanzisha uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo wa juu wa mamlaka hiyo ya dola.
Taarifa za kuanza kwa uchunguzi huo zilitangazwa na Katibu wa Bunge, Damian Foka wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Foka, madai ambayo atayafanyia uchunguzi ni yale yanayomhusisha Spika na tuhuma za kuwasilisha katika ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Bunge risiti za kughushi za matumizi yake.

“Ofisi za Bunge hazina taarifa za Spika kughushi risiti, nipeni muda niwasiliane na wakuu wa vitengo husika, ili tutafute ukweli kuhusu tuhuma hizo, na iwapo tutabaini lolote tutatoa majibu. Ile ni ofisi ya umma na mali zake zinatakiwa zitumike kwa matumizi yanayopaswa na si vinginevyo,” alisema Foka.

Pamoja na hilo, Foka alikiri madai yaliyoandikwa katika mtandao wa intaneti yanayoeleza kuwa, Sitta aliwasilisha risiti ya shilingi milioni mbili aliyonunulia dawa kutoka katika duka moja la dawa lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aidha, alisema baada ya kuwasilisha risiti hiyo, alimwelekeza alete pia cheti cha daktari kilichokuwa kikionyesha kuwa alitakiwa kutumia dawa zenye gharama hizo kutokana na matatizo yake ya kiafya katika kipindi cha wiki moja.

“Ni kweli kuwa mwezi uliopita, Spika Sitta alilipwa shilingi milioni mbili katika kipindi cha wiki moja kwa ajili ya kununulia dawa katika duka la dawa la Oysterbay,” alisema Foka.

Alisema malipo hayo ni halali kwa sababu Ofisi ya Bunge ina taarifa kuhusu matatizo ya kiafya ya Spika Sitta ambayo hata hivyo hakutaka kuyaweka bayana kwa madai kuwa maradhi ya mtu ni siri yake na daktari wake.

Hata hivyo taarifa ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kuwa, Spika amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya miguu ambayo kimsingi ndiyo aliyokuwa akiyatibu kupitia dawa alizonunua katika duka hilo la dawa.

Kuhusu madai kwamba Spika amekuwa akijihusisha katika matumizi mabaya yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake, ya magari mawili ya Bunge aliyopewa kwa shughuli zake binafsi, Foka alisema hana taarifa hizo na kuongeza kuwa uwezekano wa kuwepo kwa jambo hilo ni mdogo.

Wakati Foka akitoa taarifa hizo, maofisa kadhaa wa Bunge waliozungumza na Tanzania Daima wanaeleza kuwa, siku chache zilizopita ofisi ya Katibu wa Bunge ilipata kumhoji Sitta kuhusu kuwapo kwa madai hayo yanayomhusisha na matumizi yasiyofaa ya magari ya umma.

Foka pia alikanusha madai kwamba Ofisi ya Bunge imekuwa ikilipa gharama za umeme na maji kwa baadhi ya watu walio na uhusiano wa karibu na Spika, ambao kimsingi hawastahili kupata malipo hayo.

Pia alikanusha madai kuwa, kamati moja ya kudumu ya Bunge iligundua kuwepo mapungufu katika matumuzi ya fedha yaliyofanywa na Spika, lakini wajumbe wake walinyamazishwa na Sitta mwenyewe baada ya kuwatisha kuwa, iwapo wangeweka hadharani upungufu huo, wangekabiliwa na adhabu ya kunyimwa posho pamoja na kutopangiwa safari za nje.

Akizungumza madai kwamba Sitta amekuwa akilipwa kiasi kikubwa kwa ajili ya safari anazofanya ndani na nje ya nchi, na pia kujilimbikizia deni kubwa linalotajwa kufikia sh milioni 60, Foka alisema anachofahamu, Spika anasafiri nje na huwa analipiwa huduma ya maradhi na nusu ya asilimia 20 ya posho kama fedha za matumuzi na si zaidi ya hapo.

Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Jose Mwakasyuka ambaye alikuwapo wakati Foka akihojiwa, alisema mali za Bunge zipo salama na kwamba tuhuma zinazoelekezwa sasa kwa Spika zina kila dalili ya kuwepo nia ya makusudi ya kumchafua.

“Hizi tuhuma ni za kupakana matope na kuchafuliana majina, kwani tuhuma zenyewe hazimtaji nani aliyezitoa. Nadhani kuna watu wanataka waandishi waache kuandika mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake wajielekeze kwenye tuhuma dhidi ya viongozi,” alisema Mwakasyuka.

Hivi karibuni, Spika Sitta alizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na kueleza kuwa, hawezi kuzizungumzia kwa sababu zinatolewa na wahuni wenye lengo la kumchafulia jina lake mbele ya jamii.

Mbali ya hilo, Sitta alilielekeza Tanzania Daima kuwasiliana na maofisa wa Bunge ili kupata ukweli wote kuhusu madai hayo yaliyoandikwa katika mtandao mmoja wa intaneti.
 
"Mkjj hebu timiza usemi wako huu"
Kumbukeni yanaanzia JF yanaisha kwenye vyombo vyetu vya habari kama itakavyokuwa kesho kwenye moja ya magazeti! Wajumbe Butiama kaeni chonjo...

Umetizama ile ishu ya Spika?
 
Mkjj,
Asante kwa yote ufanyayo katika kukuza uhuru wa maoni katika awamu hii.
Heshima yako natanguliza.
Hizi tovuti na media in general are a very important weapon for
keeping these guys in check na tukinyimwa huo uhuru then we
are done!!!
Hizi ripoti za hawa mafisadi naamini asilimia kubwa ya wabongo wamezipata through such media and the least we can do is to encourage the growth of a vibrant and informed society by way of mitandao.Nimesoma mahali kwamba kuna mwana-JF mmoja alimpa mbunge f'lani fwakti za kutoka humu...mjumbe alikua hata hajui!!!

Kwa wale waosha vinywa na wapingaji madongo, acha waendelee tu
maana its all in the spirit of UHURU WA MAONI...au sio?
Ubarikiwe.

P.S. Poleni kwa msiba hapo Lansing na tuko tugeza!
 
Mzee mwanakjj,this is what they say umetuovadozi,umeandika mabo mazito sana ambayo naamini kama members watasoma hiyo article yote bila kuchoka then we can do unfogetable things in our country.Article hii ni moto wa kuotea mbali.
 
duh hapa patam.....anyway shukrani kwako MZEE MKJJ post yako imetulia na nakuahidi kuifanyia kazi pale inaponihusu...ila umesahau WAKORA.....japo umetukumbuka wasukuma...WABEJA...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom