Mirr
Member
- Jul 14, 2021
- 16
- 30
Habari wana jukwaa!
Binti mmoja alimuaga mama yake anaenda kutembelea maeneo ya kihistoria na marafiki zake. Mama yake alimjibu "safari njema mwanangu na Mungu awe nanyi"
Mtoto alimjibu mama yake "Mungu hawezi kuwa na sisi tumeshajaa tayari kwenye gari labda akae kwenye buti"
Huyo mtoto alianza safari na marafiki zake kwa gari lakini kabla ya kufika hiyo safari gari ikapata ajali wakafa wote.
Polisi walipokuja kufanya uchunguzi walikuta kwenye buti treyi ya mayai nzima haijavunjika kwasababu mungu alikuwa pamoja na iyo treyi.
Ujumbe wa hii stori
Binti alishindwa kuheshimu kauli ya mama yake wakati anamtakia kila lakheri kwenye safari yao ikiwa na maana kwamba Mungu awe nao au awaongoze kwenye safari yao, hivyo akaonesha dharau wakafa kifo kibaya cha ajali.
Waheshimu wazazi wako upate kuishi maisha marefu na yenye baraka. Wakati mwingine unaona maisha yamekuwa magumu na yenye balaa na mikosi huenda huongei ama unawadharau wazazi wako hivyo kila unachokifanya hakikisha wazazi wako hawasononeki.
Kukaa mjini pasipo kuwasaidia wazazi wako kijijini ni utovu wa nidhamu. Una miaka zaidi ya mitano hauja enda kijijini kuwaona wazazi wako au hata kuwasaidia kila kukicha upo busy na maisha yako na mke wako huwathamini wazazi kila mara wanakuongelea hakika hautafanikiwa kama hautajirudi ukawapigie goti wakuombee baraka popote unapopita uwe baraka na kupiga hatua za maendeleo hapa duniani.
Kumuona mzazi msumbufu kisa ana kupigia pigia simu ama anakuomba hela kila mara huo ni utovu wa nidhamu. Usioneshe kuchukia kwenye nafsi mzazi anapohitaji msaada kwako kwasababu hata wewe ulikuwa msumbufu wakati bado mdogo hivyo hauwezi kulipa hata robo ya wema waliokutendea wazazi wako yapaswa uwaheshimu upate kuishi maisha marefu yenye mafanikio.
Leo hii wazazi wanazika watoto kuliko watoto kuwazika wazazi,hii inadhihirisha kuwa vifo kwa watoto vimeongezeka, maisha yamekuwa mafupi kwa kukosa heshimu,utu na busara hivyo wengi hujiingiza kwenye tabia mbaya kama vile wizi, ujambazi, uvutaji wa madawa ya kulevya wanaishia kufa mapema lakini pia wengine ni laana za wazazi ambao kila muda wanasononeka kwa utovu wa nidhamu wa hawa watoto. Wahenga walishasema "asiyesikia la mkuu huvunjika guu" .Vijana tuwaheshimu wazazi kwa kufuata wanachotuelekeza tupate kuishi umri wa faida.
Hata mungu kasema katika vitabu vitakatifu kwamba hakuna mtu yoyote atakayeishi maisha marefu na yenye furaha kama hatatii wazazi wawili. Hivyo chanzo cha maisha marefu na yenye baraka hutokana na kuwaheshimu wazazi wakiwa hai. Na kama wazazi walishatangulia mbele za haki na walifariki hali yakuwa hawajakuridhia basi mlilie Mungu akuhurumie hapa duniani kwa kupata baraka zake kabla hujaondoka duniani.
Nahitimisha kwakusema, Vijana tuendelee kuwaheshimu wazazi wetu wawili kwa kuwatimizia mahitaji yote ingawa wengine tunachopata ni kidogo hivyo hivyo tukigawane huenda tutakuwa tunatengeneza maisha mazuri yenye baraka hapo baadaye, lakini pia ukiwaheshimu wazazi wako utaweza kuwaheshimu watu wengine na hii kwa vijana itasaidia hata kuleta uaminifu tunapopewa nyazifa za uongozi kuwaongoza waliotuzidi umri au tabaka lolote tutakuwa wenye busara na kuheshimu kila mtu pasipo kujikweza.
Asanteni
Miraji athumani
mirajihathuman@gmail.com