Wahindi wangefanya vipi hapa wakuu....

Wahindi wangefanya vipi hapa wakuu....

ALFMOJA

Senior Member
Joined
Sep 8, 2013
Posts
163
Reaction score
53
Inasemekana wahindi wanasaidiana sana kibiashara. Unadhani hii case study ingewahusu wahindi wangefanya vipi? Ila hapa Wanaozungumziwa ni Watanzania wenye asili ya ngozi nyesi.

Mwafrika A amepata wazo la biashara. Mtaji ni Sh. 500,000/-. Mwafrika A anazo 200,000/- tu. Tuseme mtaji hautoshi. Bidhaa inayotakiwa kuuzwa ni akili; tuseme hii ni biashara ya ujasiria akili hivi--kama vile consultancy ambayo hata hivyo itahitaji kichwa zaidi ya kimoja. Kauza wazo kwa marafiki na rafiki mmoja, Mwafrika B kasema atakubali kuchangia akili yake kama atapewa hizo 200,000/- na zingine hata akilipwa baadae ni sawa, lakini atahakikisha wazo linazaa matunda kwanza. Mwafrika A kwa kujua ujuzi wa Mwafrika B anakubali kuchukua risk. Anampa Mwafrika B 200,000/- na kazi inaanza.

Katikati ya kazi oda zimetoka na kinachotakiwa ni ufundi wa Mwafrika B ili kumonetize zile oda. Mwafrika B anaona pesa ileeeee, ishaanza kuingia. Hapa anapotea mtaani, simu za Mwafrika A anagoma kupokea.


Unadhani Wahindi wangefanyaje katika case study hii? Who is right, who is wrong, what is right, what is wrong?
 
Tatizo letu sie utapeli tuuu namaisha ya mkato.
Maana hii ngozi hata waliopo South Africa kutafuta maisha basi tunauwana sie kwa sie.
Wana apollo Mererani wakipata Mawe na wakijua unlao mara wanakuzimisha
 
Tatizo letu sie utapeli tuuu namaisha ya mkato.
Maana hii ngozi hata waliopo South Africa kutafuta maisha basi tunauwana sie kwa sie.
Wana apollo Mererani wakipata Mawe na wakijua unlao mara wanakuzimisha

pana ukweli mkuu. sema tu mie nilitamani kuichambua hii hadithi kama hapo lipo wapi? Je Mwafrika A ana tatizo? Je mwafrika B ana tatizo. kitu kama hicho. Na tatizo ni lipi?
 
Tatizo ni ubunifu......hatupendi kukaa pamoja na kulichambua soko kujua nini kinahitajika, wapi na kwa wakati gani, wengi tunarukia mradi aliobuni mwenzio na wewe unadandia, tena mbaya zaidi, badala ya kwenda mbali, pale pale jirani yake unaiga na kuanza.

Mwafrika A ni mbunifu, B ni sijui mtaalamu au msomi...au kwa kifupi mjanja njaa, alipaswa kurudi kwa A, na kumshawishi washurikiane, kwani B aliona pesa pekee, Ila A aliona mbali zaidi ya pesa, na ndo maana alirisk. Mwisho wake B atakwama mahali asione njia tena, kwani uwezo wake umeishia pale kwenye pesa tuu.
 
Back
Top Bottom