Wahindi watengeneza mifuko watoa rushwa TBS

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
Nakumbuka kikao cha wadau wa mifuko mmbadala na TBS kiliingia nyongo na hakikuisha kwa amani baada ya kutokea mvutano kati ya wabongo na wahindi waliodai wao ndio wamepewa vibali kutengeneza mifuko iliyopitishwa na serikali baada ile ya awali kuzuiliwa.

Leo TBS wanakuja na kusema hataruhusiwa mtu kuingiza mifuko nchini bila ya mifuko hiyo kua na nembo ya TBS hii ni janja janja tu ya kuhakikisha wanabana ili hawa magabachori wapate bingo hilo la kutengeneza mifuko hiyo.Wote tunajua kabisa na iko wazi mifuko iliyoruhusiwa kutumika ni material ya "Non woven bags" ambayo ni rafiki kwa mazingira.

Maoni yangu kabla TFDA nao hawaingia hapo,na NEMC nao pia nafikiri serikali ingeacha watu waagize mifuko hii kwa sharti iwe ni "Non woven material" na ipo inafahamika iache hii mambo ya kupokea rushwa tena kwa wageni jamani acheni mnatunyonga wanyonge mtatuua kama mnatafuta pesa ya uchaguzi kwa mbinu hizi hapana jamani tuna hali mbaya wanyonge.
 
Kweli shue za kata ni shida!!

Ina maana huelewi kabisa maana ya kuuza mifuko/bidhaa zenye nembo ya TBS!! Matoke yake unatuamisha wana JF wote kuwa mifuko itakayouzwa ikiwa na nembo ya TBS ni ya wahindi tena eti kwa sababu wametoa rushwa kwa watumishi wa TBS!!
 

Tulia wewe usikurupuke kujibu kama popoma.
 
Pole sana mleta mada, naona umeandika kwa uchungu mkubwa sana wallah....
 
Kuna walioagiza tayari, na waloenda physically kuleta mzigo toka China.. Hawa ndo watajua kwa nini kuku hana mkia[emoji41]
Kwani Kuna ugumu gani kuwapelekea tbs waipige hyo nembo yao?Hao wahindi wanaipelekaje huko tbs na watu weusi mshindwe kuipeleka?
 
Vitu vingine sioni kama kuna ulazima wakuanza kuagiza nje hadi mifuko mtoa mada unatak watu tuendelee kuagiza china
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…