Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kutokana uchaguzi huu ulivyokwenda, binafsi naona kuna uwezekano wa asilimia 70 mpaka 80 wa wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa, kusitisha kutoa fedha zao kwa hii serikali unless zinafanyika jitihada kubwa sana za kidiplomasia huku serikali ikilazimika kuji-commit kwa baadhi ya mambo: demokrasia, utawala bora na kuheshima haki za binadamu, vinginevyo tutalimia meno.
Katika kulimia meno huko, ni pale tutapolazimika kuongezea makusanyo na kubana matumizi kufidia nakisi itayotokana na kukosekana kwa fedha za wahisani.
Nini kinaweza kutokea?
Kwasababu hakuna vyanzo vipya vya mapato, uwezekano uliopo ni kuongeza wigo wa kodi kwa wafanyabiashara na hata wafanyakazi, na serikali kulazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu, basi hata sitting allowance za wabunge zinaweza kuguswa huko mbeleni.
Tukumbuke tuna deni la Taifa tunalohitaji kulihudumia kila mwezi, na wakati huo huo, tuna miradi ya matrilioni inayotakiwa kukamilika katika ungwe hii ya mwisho ya Mzee Baba na sidhani kama atakubali kushindwa kuikamilisha labda akosa hela kabisa.
Na ikitokea anakosa hela kabisa, basi wewe mwananchi wa kawaida jiulize utakuwa katika hali gani na pia jiulize kama elimu bure nayo itaendelea.
Naishia hapo, wache nisepe zangu kuelekea shambani mvua zimeanza.