Wahisani wakibana kisawasawa, mbali na Wafanyabiashara kukamuliwa, hata sitting allowance za Wabunge zinaweza kutoweka

Acheni hizi akili za kipumbavu na za kinafiki za kujifanya nyinyi ni sehemu ya jamii mkiwa hadharani halafu gizani mnaendekeza fitina.

Zitto Kabwe na Lissu wanakwenda kupotea kisiasa kwa sababu ya kuendekeza hulka hizi za kipumbavu. Ni hulka zisizoweza kufanikiwa hata mara moja.

Wahisani wana maslahi yao ya kiuchumi humu nchini hawawezi kuwaamini watu ambao hawana majukumu halali ya kuongoza nchi.

Hawawezi kuwaamini watu wasiokubalika mbele ya jamii ya kitanzania sana sana watawatumia tu na baadae watawapuuza mazima.
Duniani lazma kuwepo watu wenye roho mbaya sana kama hii ili ukombozi ufikiwe...

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Itabidi safari hii nchi iendeshwe kijambazi na kidukuzi kama North Korea maan a hamna jinsi
 
Kutoka na uchaguzi huu ulivyokwenda, binafsi naona kuna uwezekano wa asilimia 70 mpaka 80 wa wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa, kusitisha kutoa fedha zao kwa hii serikali unless zinafanyika jitihada kubwa sana za kidiplomasia huku serikali ikilazimika kuji-commit kwa baadhi ya mambo: demokrasia, utawala bora na kuheshima haki za binadamu, vinginevyo tutalimia meno.

Katika kulimia meno huko, ni pale tutapolazimika kuongezea makusanyo na kubana matumizi kufidia nakisi itayotokana na kukosekana kwa fedha za wahisani.

Nini kinaweza kutokea?

Kwasababu hakuna vyanzo vipya vya mapato, uwezekano uliopo ni kuongeza wigo wa kodi kwa wafanyabiashara na hata wafanyakazi, na serikali kulazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu, basi hata sitting allowance za wabunge zinaweza kuguswa huko mbeleni.

Tukumbuke tuna deni la Taifa tunalohitaji kulihudumia kila mwezi, na wakati huo huo, tuna miradi ya matrilioni inayotakiwa kukamilika katika ungwe hii ya mwisho ya Mzee Baba na sidhani kama atakubali kushindwa kuikamilisha labda akosa hela kabisa.

Na ikitokea anakosa hela kabisa, basi wewe mwananchi wa kawaida jiulize utakuwa katika hali gani na pia jiulize kama elimu bure nayo itaendelea.

Naishia hapo, wache nisepe zangu kuelekea shambani mvua zimeanza.
Mnakoekea ni kwenda kwa waganga ili mroge bunge lijae upupu kwenye viti ili wabunge wasiwe wanakaa. Kwani ilikuwa lazima watanzania tuchague Ccm? Bajeti ya 2019- 2020 wahisani walichangia % ngapi? Acha kuwa na fikra potofu.
 
Nchi hii tajiri,hakuna haja ya kubana,kwanza wazungu wanatuogopa sana,hawawezi kubana chochote,,
 
Haya pia tuyaongee miaka mitatu baadae. Tanzania is very unique. Msichanganye Tanzania na mauzauza mengine
 
Aah wapi, tutakuwa masikini wote lakini sio wabunge, anataka wabunge wawe mabilionea.

Jamaa ana kichwa cha tofauti sana na wengine.
 
Kutoka na uchaguzi huu ulivyokwenda, binafsi naona kuna uwezekano wa asilimia 70 mpaka 80 wa wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa, kusitisha kutoa fedha zao kwa hii serikali unless zinafanyika jitihada kubwa sana za kidiplomasia huku serikali ikilazimika kuji-commit kwa baadhi ya mambo: demokrasia, utawala bora na kuheshima haki za binadamu, vinginevyo tutalimia meno.

Katika kulimia meno huko, ni pale tutapolazimika kuongezea makusanyo na kubana matumizi kufidia nakisi itayotokana na kukosekana kwa fedha za wahisani.

Nini kinaweza kutokea?

Kwasababu hakuna vyanzo vipya vya mapato, uwezekano uliopo ni kuongeza wigo wa kodi kwa wafanyabiashara na hata wafanyakazi, na serikali kulazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu, basi hata sitting allowance za wabunge zinaweza kuguswa huko mbeleni.

Tukumbuke tuna deni la Taifa tunalohitaji kulihudumia kila mwezi, na wakati huo huo, tuna miradi ya matrilioni inayotakiwa kukamilika katika ungwe hii ya mwisho ya Mzee Baba na sidhani kama atakubali kushindwa kuikamilisha labda akosa hela kabisa.

Na ikitokea anakosa hela kabisa, basi wewe mwananchi wa kawaida jiulize utakuwa katika hali gani na pia jiulize kama elimu bure nayo itaendelea.

Naishia hapo, wache nisepe zangu kuelekea shambani mvua zimeanza.
unaota ndoto ya mchana wewe😂😂😂 yani posho ikose kisa mbowe na lissu hawana jimbo😂😂😃😃?????
 
Hivi wakibana Nani kati yetu atakuwa na hali nzuri.. Tuombe serikali itafakari hili ije na mustakabali ambao hautamuumiza mwananchi...

Siyo kusema wajamaa wabane...
 
Kutokana uchaguzi huu ulivyokwenda, binafsi naona kuna uwezekano wa asilimia 70 mpaka 80 wa wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa, kusitisha kutoa fedha zao kwa hii serikali unless zinafanyika jitihada kubwa sana za kidiplomasia huku serikali ikilazimika kuji-commit kwa baadhi ya mambo: demokrasia, utawala bora na kuheshima haki za binadamu, vinginevyo tutalimia meno.

Katika kulimia meno huko, ni pale tutapolazimika kuongezea makusanyo na kubana matumizi kufidia nakisi itayotokana na kukosekana kwa fedha za wahisani.

Nini kinaweza kutokea?

Kwasababu hakuna vyanzo vipya vya mapato, uwezekano uliopo ni kuongeza wigo wa kodi kwa wafanyabiashara na hata wafanyakazi, na serikali kulazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu, basi hata sitting allowance za wabunge zinaweza kuguswa huko mbeleni.

Tukumbuke tuna deni la Taifa tunalohitaji kulihudumia kila mwezi, na wakati huo huo, tuna miradi ya matrilioni inayotakiwa kukamilika katika ungwe hii ya mwisho ya Mzee Baba na sidhani kama atakubali kushindwa kuikamilisha labda akosa hela kabisa.

Na ikitokea anakosa hela kabisa, basi wewe mwananchi wa kawaida jiulize utakuwa katika hali gani na pia jiulize kama elimu bure nayo itaendelea.

Naishia hapo, wache nisepe zangu kuelekea shambani mvua zimeanza.
Watu kama nyie ndio hamnazo akili kabisa. Mumeaminishwa kwamba bila wahisani nchi haiendi. Hebu kwanza kama mna uwezo fanyeni utafiti muone kama ni kiasi gani cha grants kama hamkuona ni kidogo sana. Kama ni mikopo kukopesha ni biashara ziko nchi na mabenki kibao tunaweza kukopa sio lazima ulaya. Nchi hii haishtuki kutishiwa misaada ili iuze uhuru wake. Huko tulishatoka zamani. Ni vibaraka tu waliyoleweshwa kasumba na mabeberu kama lissu ndio wanaendelea kutishia nchi nyau wa kizungu.
 
Bado unabisha?
Mafuta yatapanda bei mara dufu, uzalishaji utashuka, kodi zitapanda sana, bei zitapanda sana, maisha yatakuwa magumu. Hapo ndipo kila mtu ataelewa umuhimu wa wale mnaowaita mabeberu. Muda utaongea. Ukweli ni kwamba tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyotuhitaji.
 
Watu kama nyie ndio hamnazo akili kabisa. Mumeaminishwa kwamba bila wahisani nchi haiendi. Hebu kwanza kama mna uwezo fanyeni utafiti muone kama ni kiasi gani cha grants kama hamkuona ni kidogo sana. Kama ni mikopo kukopesha ni biashara ziko nchi na mabenki kibao tunaweza kukopa sio lazima ulaya. Nchi hii haishtuki kutishiwa misaada ili iuze uhuru wake. Huko tulishatoka zamani. Ni vibaraka tu waliyoleweshwa kasumba na mabeberu kama lissu ndio wanaendelea kutishia nchi nyau wa kizungu.

'Kama ni mikopo kukopesha ni biashara ziko nchi na mabenki kibao tunaweza kukopa sio lazima ulaya.'

Zimbabwe mpk leo haijapata hayo mabenki ya kuikopesha sio?
 
Back
Top Bottom