KATIKA kile kinachoweza kutafsiriwa kama ukosefu wa umakini katika sektaya elimu nchini, Shule Kuu ya Uhandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC)ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), juzi ilifanya kituko cha mwaka kwakuwatunuku shahada wahitimu wasiostahili.
Katika mahafali hayo ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika juzi, wanafunziwawili; Jongo Nasra na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Oliver,walitunukiwa shahada ya awali ilhali wakiwa si wahitimu stahiki.
Makosa hayo ambayo kimsingi yalianzia kwenye Idara ya Taaluma ya chuohicho, bado hayakuweza kugunduliwa na Mkuu wa Shule hiyo, Dk. Hubert Makoye, nahivyo kuwatambulisha wahusika kwa Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Flugence Kazura,ili watunukiwe shahada hizo.
Hatua hiyo iliwashangaza baadhi ya wahitimu na wanachuo wenginewanaowafahamu watajwa, kusikia wakihudhurishwa kuwa wamefaulu na hivyo wanasifa za kutunukiwa shahada.
"Wafuatao wamefaulu na wana sifa za kupewa shahada, hivyo nawahudhurishakwako watunukiwe shahada ya awali ya habari na mawasiliano ya umma," alisemaDk. Makoye mbele ya Mkuu wa chuo baada ya kusoma majina ya wahitimu.
Hata hivyo, baada ya minong'ono na miguno ya wanachuo, Tanzania Daimalilidodosa kutaka kujua ni kwanini imejitokeza hali hiyo, ndipo ikabainika kuwawatajwa hawakuwa wahitimu.
"Nasra alisoma mwaka wa kwanza kisha akaahirisha masomo na mwaka wa pilialisoma muhula mmoja halafu akaacha kabisa, hivyo hayupo tena chuoni," kilisemachanzo chetu.
Tanzania Daima pia ilielezwa kuwa, Oliver naye alipata matatizo yakiafya akawa ameahirisha masomo, na kwamba baadaye aliendelea na sasa yupomwaka wa tatu.
Hata hivyo, licha ya majina hayo kuingizwa kimakosa katika orodha yawahitimu wenye sifa za kutunukiwa shahada, bado uongozi haukuweza kubainimkanganyiko huo na hivyo, Nasra na Oliver kutambulika kama sehemu ya wahitimuwaliotunukiwa shahada ya awali.
Juhudi za kumtafuta Mkuu waSJMC, Dk. Makoye, hazikuweza kuzaa matunda kwa siku ya jana ili aweze kufafanuajuu ya mkanganyiko huo wa kuhudhurisha majina ya wahitimu wasiostahili iliwatunukiwe shahada.
My TAKE:
Wale ambao wandhani wamesimama, kumbe wameshaanguka siku nyingi.