A
Anonymous
Guest
Sisi Wahitimu tuliomaliza masomo yetu kati ya mwaka 2014 na 2019 tunaomba Sekretarieti ya Ajira izingatie utaratibu wa kutenga au kugawanya baadhi ya nafasi za ajira kati ya wahitimu wa muda mrefu na wahitimu wa karibuni. Hatua hii itasaidia kutoa fursa sawa kwa Watanzania wote wanaotafuta ajira.
Kwa sasa, sisi wahitimu wa zamani tunakumbana na changamoto ya kupata nafasi za kazi kwa kuwa katika baadhi ya usaili, wahitimu wa karibuni huwa na kumbukumbu na uelewa wa masomo yao ulio hai zaidi kutokana na muda mfupi tangu walipohitimu. Tunaiomba Serikali na Sekretarieti ya Ajira kulifanyia kazi suala hili ili kuhakikisha usawa wa fursa kwa wahitimu wote bila kujali mwaka waliomaliza masomo yao.
Tunaamini hatua hii itasaidia kuongeza usawa na haki katika mchakato wa ajira nchini.