Wanafunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Iringa tunapenda kuwasilisha malalamiko yetu kuhusu ongezeko la gharama zinazotozwa wakati wa kuchukua vyeti, ambazo kwa sasa zimekuwa mzigo mkubwa kwa wengi wetu.
Chuo kimeweka gharama ya Shilingi 100,000/= kwa ajili ya kusaidia mchakato wa uhamishaji wa taarifa kutoka mfumo wa zamani wa SAMIS kwenda mfumo wa SIMS, ambapo fedha hizo zinaelezwa kuwa zitatumika kumlipa mtu atakayehusika kuingia kwenye mfumo na kufuatilia matokeo ya wanafunzi.
Changamoto iliyopo ni kwamba mabadiliko ya mfumo yalifanywa na uongozi wa chuo, lakini gharama zake zinaonekana kuhamishiwa kwa wanafunzi ambao hawakuhusika na maamuzi hayo. Hali hii imekuwa ikiwafanya wahitimu wengi kushindwa kuchukua vyeti vyao kutokana na kushindwa kumudu gharama hizo.
Wakati huohuo, wahitimu wengi bado hawana ajira na wanategemea vyeti hivyo kuomba nafasi mbalimbali za kazi au kuendelea na hatua nyingine za kimaendeleo. Kuongezewa gharama ambazo hawakuzipangilia kunazidi kuwaweka katika mazingira magumu.
Tunaomba uongozi wa Chuo Kikuu cha Iringa na mamlaka husika kulifanyia kazi suala hili, kupitia upya gharama hizo na kuhakikisha wanafunzi hawabebeshwi mzigo wa mabadiliko ya mifumo yaliyofanywa na taasisi yenyewe.
Tunahitaji suluhisho litakalowezesha wahitimu kupata vyeti vyao bila vikwazo vya gharama zisizo na uwezo wa kuzimudu.
==========================
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Iringa tuliomaliza masomo kuanzia mwaka 2024 kurudi nyuma tunalazimishwa kutozwa kiasi cha takribani Sh 100,000 kwa ajili ya kupata transcript zetu.
Pamoja na kutakiwa kulipa kiasi hicho, tunaambiwa tufuate taratibu mbalimbali ikiwemo kuandika barua na kuziwasilisha katika idara husika ili taarifa zetu za kitaaluma na nyaraka nyingine zitafutwe.
Hii changamoto imeanza baada ya Chuo kuhamisha mfumo wa kuhifadhi taarifa za wanafunzi kutoka SAMIS kwenda SIMS, ambapo taarifa zote za wanafunzi tuliomaliza 2024 kurudi nyuma hazikuhamishwa kwenda kwenye mfumo mpya hivyo kulazimishwa kufanya malipo hayo na kulipia cheti 65000/=.
Kwahiyo tunatakiwa kulipia gharama za utafutaji na uchakataji wa taarifa zetu ili waweze kupata transcript.
Sisi tunataka kujua kwanini tuingie kubeba gharama zinazotokana na mabadiliko ya mfumo wa ndani wa chuo, wakati tayari tulishamalizaga chuo na tulikamilisha masomo yetu na taratibu zote za kitaaluma.
Lakini pia transcript ni nyaraka ya kitaaluma ambayo hutolewa bila malipo yoyote, sasa kwanini kututoza kiasi hicho cha fedha ili tuioate?