A
Anonymous
Guest
Sisi wahitimu wa kozi ya Renewable Energy Technology kutoka vyuo mbalimbali tunakabiliwa na changamoto tunapoomba ajira kupitia mfumo wa Ajira Portal.
Licha ya kuwa tulisomea teknolojia ya nishati jadidifu inayohusiana na sekta ya umeme, tunapoitwa kwenye usaili wa nafasi za kazi zinazohusiana na umeme, baadhi yetu tunaambiwa kuwa kozi tuliyosomea haitambuliki kama kozi ya umeme. Hali hii inatunyima fursa ya kushiriki katika usaili na kupata ajira kulingana na taaluma yetu.
Tunaomba uongozi wa Utumishi wa Umma pamoja na mamlaka husika kupitia upya suala hili na kutoa ufafanuzi kuhusu utambuzi wa kozi ya Renewable Energy Technology katika nafasi za ajira za sekta ya umeme.
Ni muhimu kuweka wazi sifa na vigezo vinavyotumika ili wahitimu wa kozi hii wapate fursa ya kuomba na kushiriki katika usaili wa nafasi wanazostahili kitaaluma.
Tunaomba suala hili liangaliwe kwa umakini, kwani limekuwa changamoto kubwa kwa wahitimu wengi wa kozi hii wanaotafuta ajira.