KERO Wahitimu wa Diploma katika Chuo cha Mipango Campus ya Mwanza tunachelewa kupata vyeti

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wanafunzi tuliomaliza masomo ya Diploma tunaomba msaada kuhusu changamoto ya kucheleweshewa vyeti vyetu.

Kila tunapofika chuoni kufuatilia vyeti, tunaambiwa kuwa mashine ya kuchapisha au kutoa vyeti imeharibika. Hali hii imetuletea usumbufu mkubwa, hasa kwa wale wanaotoka maeneo ya mbali ambao hulazimika kutumia gharama za usafiri na kuendelea kugharamia makazi wakati wakisubiri huduma hiyo.

Tunaomba uongozi wa chuo ufuatilie na kutatua changamoto hii kwa haraka ili wahitimu waweze kupata vyeti vyao kwa wakati na kuendelea na hatua nyingine za maisha na ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…