KERO Wahitimu wa Diploma Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mwaka 2023 tunazungushwa kupata cheti mpaka leo

KERO Wahitimu wa Diploma Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mwaka 2023 tunazungushwa kupata cheti mpaka leo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba mnisaidie kupaza sauti kuhusu changamoto inayowakabili wahitimu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE), hususan wanafunzi wa Diploma in Adult Education.

Mimi ni mwalimu niliye kazini, nilihitimu mwaka 2023 Kampasi ya Bukoba. Hata hivyo, hadi sasa bado sijapatiwa cheti changu cha kuhitimu, jambo ambalo limekuwa likinikwamisha katika maendeleo yangu ya kitaaluma na kikazi.

Nilipofuatilia kujua chanzo cha ucheleweshaji, nilielezwa kuwa kulikuwa na tatizo lililosababisha matokeo kuchelewa, lakini tatizo hilo lilishatatuliwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Pamoja na hilo, hadi leo hakuna taarifa rasmi kuhusu lini vyeti vitatolewa.

Kila ninapofuatilia, jibu ninalopewa ni kwamba "subirini majina yatatumwa", lakini hakuna mwelekeo wala ratiba inayoonyesha ni lini orodha hiyo itatolewa. Hali hii inatuacha gizani na kutufanya tushindwe kupanga maendeleo yetu.

Kinachoumiza zaidi ni kuona wanafunzi waliokuja baada yetu wanahitimu na kupata vyeti vyao kwa wakati, ilhali sisi tuliomaliza mwaka 2023 bado tunaendelea kusubiri bila majibu ya kueleweka.

Napenda kusisitiza kuwa hii si changamoto yangu pekee. Wapo wahitimu wengine wengi wa Diploma ya Elimu ya Watu Wazima, hasa walimu wanaojiendeleza kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, wanaokabiliwa na tatizo hili.

Tunaiomba Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoa ufafanuzi kuhusu: Sababu za kucheleweshwa kwa vyeti vya wahitimu wa mwaka 2023, hatua zilizochukuliwa kutatua tatizo hili na ratiba rasmi ya kutolewa kwa vyeti vya wahitimu wote walioathirika.

Tunahitaji vyeti hivi kwa ajili ya kuthibitisha sifa zetu, kujiendeleza kitaaluma, kupata fursa za kazi na kupandishwa madaraja. Tunaomba mamlaka husika zilichukulie suala hili kwa uzito na kutoa majibu ya wazi kwa wahitimu wote walioathirika.
 
Back
Top Bottom