RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara 32:
Lipo kundi la vijana waliohitimu elimu ya juu ambao watazeeka bila hata kumiliki viwanja vya kujenga nyumba ambavyo kwa sasa vinapatikana hadi kwa Tsh 1,000,000. Ni kwasababu kundi hili la vijana wenye elimu za juu wanasubiri ajira za ofisini zitakazoendana na GPA zao za vyuoni. Hawataki kufanya kazi halali za kutoka jasho, wanasubiri kazi za kwenye viyoyozi.
Wapo baadhi ya wahitimu wa elimu ya juu wanajishughulisha na kazi ndogo ndogo za mitaani pasipo kutazama elimu zao, hakika wapewe maua yao. Lakini wengi waliohitimu elimu za juu wapo mtaani hawataki kujishughulisha, mbaya zaidi huwadharau vijana wenzao ambao wanatafuta pesa kupitia kazi halali ndogo ndogo.
Naongea na wewe mhitimu wa elimu ya juu; dharau yako ndio inakufanya mpaka sasa huna kibarua cha kukuingizia pesa, huna mtaji, huna hata senti tano mfukoni, kwa ujumla huna mbele wala nyuma licha ya kuwa una vyeti vya elimu ya juu. Vijana wengi wanaojiita wasomi kitu pekee wanachomiliki ni smartphone walizotoka nazo vyuoni kwa pesa ya Boom.
Na hao ndio vijana ambao kutwa hawamalizi kulalamika kupitia comments za social media huku wakiwa wamekaa vijiweni au ufukweni. Si kwamba wanalalamika kwasababu ya fikra pana walizonazo bali ni njaa za kujitakia wenyewe, yes! ni njaa. Akitokea mbunge au waziri yoyote akiwaambia; "vijana mliohitimu elimu ya juu anzeni kujiajiri" - watampinga kwa comments nyingi za kejeli na matusi, kamwe hawataki kuukubali ukweli kwamba nafasi za kuajiriwa ni chache kuliko wingi wao, hii ni kwasababu kila mhitimu wa elimu ya juu ana ndoto ya kuwa waziri.
Akikutana na ujumbe mtandaoni usemao EWE MSOMI JIAJIRI, atachukua iphone yake aliyoinunua kwa Tsh 3,500,000 kisha atacomment; "Mtaji wa kujiajiri uko wapi, mbona wewe hukujiajiri" - asijue kwamba simu yake ni mtaji tosha.
Wahitimu wengi wa elimu ya juu hata kama watapewa mashamba ya bure, mbegu za bure, mashine za umwagiliaji, na mbolea za bure kamwe hawatoweza kulima - utamsikia; "sikusomea kulima nimesomea uhasibu" - yaani wanasubiri viti vya maofisini tu.
Right Marker
Dar es salaam